Sunday, October 22, 2017

JUMAPILI NJEMA NDUGU ZANGUNI BARAKA ZA MWENYEZI MUNGU ZIWE PAMOJA NANYI....

Walio wengi hudhani Baraka za Mungu ni kufanikiwa kimaisha pekee, kumbe hata kuiona siku ya LEO ukiwa mzima ni Baraka na Neema yake.
JUMAPILI NJEMA KWA WOTE NA BARAKA, FURAHA NA AMANI VITAWALE NDANI YA MIOYO YENU .

2 comments:

  1. Maisha ni zawadi si haki
    Hata uwe maridadimwenzio usidhihaki
    Wote kule tutarudi kwa furaha hata dhiki
    Maisha ukifaidi umshukuru Maliki
    Kwani siku ya kurudi wote ni kindakindaki

    Ukiona wapumua jua wapo wenye haki
    Hawakuliona jua tofauti na waso haki
    Hakuna anayejua vipimo vyake el Shaddai
    muhimu ni kutambua kuwa hakuna unachodai
    Kwa kila unapumua ni sababu ya al Muta'aali

    Pumzi unayovuta ni yake Hamiydu
    Na mali unayopata ni yake al Muyidu
    Maringo unayonata ni yake al Maajidu
    Mateso unayopata anayajua Assamadu

    ReplyDelete
  2. Duh! kaka Mhango umeyapatia madhaifu yangu ahsante. Na kweli ulichosema ni kweli yabidi tukumbushane....

    ReplyDelete