Nikiangalia mti napata taswira ya watu wanaotuzunguka katika maisha yetu. Kama ujuavyo mti, huwa kuna majani, matawi na mizizi. Vivyo hivyo watu wanaotuzunguka, wapo ambao ni majani, wapo ambao ni matawi na pia wapo ambao ni mizizi. Kuna watu wanakuja katika maisha yetu kama majani kwenye mti. Huwa wapo kwa msimu tu, huwezi kuwategemea muda wote, kwa sababu wao ni dhaifu. Ila wapo kwa ajili ya kutoa kivuli. Hivyo si wakuwapuuza. Kama yalivyo majani kwenye mti wapo kwa ajili ya kunyonya chochote kutoka kwako. Nakufanya wapendeze kisha wachanue maua mazuri. Lakini kuna kipindi cha kiangazi kikifika jua huwa, ni kali na upepo makali wao hunyauka na kupeperushwa na upepo huondoka na kukuacha mpweke. Huwezi kuwalaumu kwa kuwa hivyo ndivyo walivyoumbwa.
Aina ya pili wa watu wanaotuzunguka ni kama matawi kwenye mti wao huhimili vishindo kuliko majani, watakuwa na wewe katika kipindi kirefu katika maisha yako. Ukipata misikitiko mikali mara mbili au tatu ni rahisi kuwapoteza. Mara nyingi hawa huwa na subira. Lakini hali ikiwa ngumu sasa sana hukuacha mpweke, ingawa wana msikamano kuliko majani. Unatakiwa kuwachambua sana kabla hujawekaeza muda wako mwingi kwao. Lakini, usiwalaumu kwa kuwa hivyo ndivyo walivyoumbwa.
Aina ya tatu ni watu wanaokuja kwako kama mizizi kwenye mti ukiwapata hawa shukuru MUNGU ni vigumu kuwaona au kuwapata huwa hawajionyeshi. Kazi yao ni kushikilia usianguke, uweze kufanikiwa na kuishi maisha yenye afya na furaha tele. Unapofanikiwa hukutakia mafanikio zaidi, hukaa nyuma ya pazia, na hawatoi nafasi kwa walimwengu kugundua kuwa wapo kwa ajili yako. Ukipata mitikisiko mikali katika maisha yako huvumilia na kuishi na wewe hadi mwisho. Chochote kikikutokea kiwe kibaya au kizuri wao wapo. Kama ulivyo mti una majanai mengi, matawi mengi, lakini mizizi michache sana na ni vigumu kuiona.
Tuangalie maisha yetu kuna matawi na majani mangapi yanayotuzunguka, Na je? kuna mizizi mingapi? Na swali la mwisho ambalo pia ni muhimu je? wewe ni nani kwa watu wanaokuzunguka?
samahani niliwahi kuona clip yake naiomba kama unayo
ReplyDelete