Tupo wengi sana tunaofikiri hivi:-Ya kwamba kuna mambo mengi sana tunapitia katika maisha yetu ya kila siku mengine mazuri, na mengine mabaya na wakati mwingine tunakutana na watu wazuri ambao wana tufurahisha lakini wakati huohuo yawezekana ukakutana na mtu ambaye akakuumiza sana moyo wako iwe ni kazini, nyumbani au katika mahusiano.
Jambo la muhimu ni kujua namna ya kukabiliana na changamoto zote nzuri na mbaya, kwani ukiweka moyoni yale yanayo kuumiza huwezi kusonga mbele, ila ukiamua kusahau nakufanya juhudi katika maendeleo yako, basi utafanikiwa hata wahenga walisema " SAHAU YALIYOPITA UGANGE YAJAYO".
PANAPO MAJALIWA NDUGU ZANGUNI!
Asante kwa ujumbe mzuri Kadala wa mimi
ReplyDeleteMungu aendelee kukutumia
mingilove kutoka kwa Kachiki
Kachiki ...nafurahi umeupenda ujumbe nami pia nakutakia uwe na afya njema na mingilove kutoka kwa kadala wako.
ReplyDelete