Tuesday, April 5, 2016

MADENGE ATAKA KUMPOSA BIBI YAKE KWA VILE BIBI ANAMWITA MCHUMBA....

Leo nimekumbuka  kitu ni kwamba babu yangu alipenda sana kuniita mchumba Wake na pia bibi yangu alikuwa akiwaita kaka zangu wachumba zake. Nilikuwa nikijiuliza sana inakuwaje  hii? Nilipata maelezo kiasi na nikaridhika ingawa ilinipa sana utata. Haikuishia hapo kulikuwa na  dereva mmoja  ambaye alikuwa rafiki wa familia naye alipenda sana kuniita mchumba hapo ndio nikabaki nimechanganyikia kabisa, nadhani nilichanganyikiwa kama MADENGE...hebu msome yeye alivyowaza kuhusu bibi yake..... Si mnakumbuka hadithi  ya Madenge darasa la .....

Je? hapa ni utata wa lugha au ndiyo mila na desturi zetu?  WOTE MNAPENDWA NA TUPO PAMOJA!!

2 comments:

  1. Madenge alikuwa bonge ya thinker ambaye alikuwa mahiri katika kurahisisha mambo. Unamuwowa mama yangu nami namuwowa mama yako. Utoto kweli raha. Madenge -kama mtoto yeyote -alikuwa na namna yake ya kutathmini na kudurusu mambo. Kuna somo kubwa hapa. Najaribu kufikiri namna nitakavyomjibu kamanda wangu atakaponijia akitaka kumuwowa mama yangu. Nitamjibu kuwa mimi si baba wa mama yangu. Hivyo, siwezi kuwa na comment.

    ReplyDelete
  2. Kaka Mhango ...inabidi ujiandae. Ila kwa kweli kuwa mtoto ni raha sana na pia mara nyingine huwa sijui wanaelewa maana yake ?

    ReplyDelete