Monday, March 7, 2016

JUMATATU HII TUANZE HIVI! MUHIMU:- FAIDA KUMI ZA KUNYWA MAJI MOTO YENYE LIMAO KILA UNAPOAMKA

1. Huongeza kinga yako ya mwili hasa kupambana na magonjwa madogo madogo kama vile mafua  na kikohozi kutokana na kuwa na vitamini C
2. Husafisha mfumo wako wa chakula, kuondoa sumu mwilini na kuzuia gesi kujaa tumboni mara kwa mara.
3. Huleta hewa safi kinywani.
4. Hukuongezea uchangamfu na kufanya siku yako ianze vizuri sana.
5. Husaidia majeraha kupona kwa haraka kutokana na kuwa (ascorbic acid) asidi  ya kutosha. Pia huimarisha mifupa.
6. Husaidia mmengènyo wa chakula utakachokula asubuhi au mchana kwa kuondoa vikwazo vyote vinavyoweza kuzuia umengényaji wa chakula.
7. Huimarisha ngozi yako, kuondoa makunyanzi na kukupa muonekano mzuri.
8. Husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uzito kwani maji moto ya limao huyeyusha mafuta ya kutosha
9. Huyapa macho yako afya nzuri na kuimarisha kuona
10. Huondoa hali ya kuhitaji kahawa kila asubuhi ambayo si nzuri kiafya.

4 comments:

  1. Da Yasinta asante sana kutupatia dawa ya bure na yenye faida kwenye mwili. Nataka kujua maji yawe ya moto au vuguvugu na badala ya limao huwezi kutumia ndimu? Asante. By Salumu.

    ReplyDelete
  2. Asante sana dada,,,,,faida kede kede kwakweli

    ReplyDelete
  3. Kaka Salumu! Maji yawe ya moto kama vile maji ya Chai na unaweza ukatumia ndimu badala ya limao.

    Ester! Karibu sana...

    Kaka Ray! Na chilawu mewawa!

    ReplyDelete