------------------------------------------------------------------------------------------------------------
YUPO NDANI YA MSONGO MKALI
Shirika la Afya Dunian (WHO) linaeleza kwamba, msongo ndiyo utakaokuwa unashika nafasi ya pili kwa kusababisha vifo kwa watu katika nchi zinazoendelea kufikia mwaka 2020. Siyo vifo tu bali hata kusababisha kuondoka kwa uwezo wa watu katika kuwajibika.Kwa sasa zaidi ya watu milioni 340 duniani wanasumbuliwa na msongo. Kwa ujumla tatizo hili limevuruga zaidi ya moja kwa kumi (10%) ya muda wa uzalishaji duniani. Zaidi ya nusu ya wale wenye tatizo hili huwa hawajui kwamba wanalo na hata walio karibu yao kiuhusiano huwa pia hawajui kwamba, wenzao wako kwenye tatizo. Je, sisi tuko kwenye usalama kiasi gani? Je, tunajua au hatujui kwamba tuko kwenye kusongeka? Na tukijua kwamba tunalo tatizo hilo tutatoka vipi?...
Mara nyingi tunakereka, kuvunjika moyo, kuhuzunika na kusononeka, lakini maisha yanaendelea, hayasubiri. Kipitia kusononeka na kusongeka kwwenye maisha tunapoteza uwezo wetu wa kuiona na kuikubali hali halisi na hatimaye pia tunaweza kupateza maisha yetu....
Hebu tuangalie baadhi ya dalili zifuatazo ambazo huwa zinatusumbua katika msongo:-
*Kuwa kwenye huzuni ya muda mrefu kunahesabiwa kama dalili ya sononi.
*Kukosa nguvu kwa maana ya mtu kuhisi hana uwezo wa kufanya shughuli au mambo mengi.
*Kupoteza matumaini na hisia kwamba mtu hana thamani.
*Kushindwa kufurahia mambo au shughuli zile ambazo hapo nyuma mtu alikuwa anazifurahia.
*Kushindwa kuzingatia mambo, iwe masomo, mazungumzo au shughuli.
*Kulia bila sababu za msingi na pengine kukosa au kushindwa kuzuia uliaji huo.
* Ugumu katika kufanya uamuzi wa aina yoyote hata ule mdogo au unaohusu mambo madogo
madogo.
* Kuhisi kukosa amani na kuwa kama vile mtu anawashwa kwenye hisia zake, hivyo kuhisi kukereka
tu.
*Kulala kwa ziada, yaani kuwa na ongezeko la kiwango cha usingizi. Tunasema, kulala-lala. Lakini
kwa wengine, badala ya kuwa na usingizi wa ziada, hupoteza usingizi kabisa. Hivyo, tunasema
kukosa usingizi.
*Maumivu ya maeneo mbalimbali ya mwili ambayo hayana maelezo ya chanzo chake hasa.
*Matatizo ya tumbo, hasa udhaifu wa usagwaji wa chakula. Kukosa choo huweza kujitokeza.
*Kupungukiwa na hamu ya tendo la ndoa kwa kiwango kikubwa.
*Kuumwa na kichwa mara kwa mara na wakati mwingine kwa kiwango kikubwa.
*Kubadilika kwa hamu ya kula na mara nyingi kupoteza hamu ya kula kunakopelekea udhaifu wa
mwili.
*Kuwa na mawazo ya kutaka kujiuwa kwa sababu mtu haoni kwa nini aishi. Wengine wanaofanya
majaribio ya kujiuawa huwa wanakabiliwa na kusongeka kimaisha.
PANAPO MAJALIWA!
Hivi karibuni nilikutana na kijana mmoja kutoka Bukoba na anieleza mambo ya kutisha aliyokutana nayo katika msongo wa maisha.Tunaishi na misongo ya maisha na kila mmoja wetu anahitaji kitia moyo kutoka kwa mwenzake.
ReplyDeleteKaka Ray...ama kweli misongo inazidi kwa kasi mno kama ulivyosema ni MUHIMU SANA KUTIANA MOYO na chochote kinachokusibu usisite kumweleza aliye karibu nawe maana ukizidi kukaa nalo moyoni itakuumiza tu na hata mwisho Wake kuishia kupoteza maisha. TUWE WAWAZI.
ReplyDelete