Thursday, February 11, 2016

SONGEA: MPUNGA WATUMIKA KUTENGENEZEA POMBE!

Pombe inayotokana na mpunga ikiandaliwa kwa kuchemshwa

Ubovu wa Barabara katika kijiji cha Ifinga Kata ya Matumbi  Wilaya ya Songea katika Mkoa wa Ruvuma, unasababisha mpunga kutengeneza pombe ya kienyeji.
Pombe hiyo ijulikana kama pombe ya mpunga, inachangwanya kwa mapumba laini ya mpunga,  kwa kuyaloweka kwa siku tatu, pia wanachanganya na uji wa ulezi uliolowe kwa kwa siku tatu.

Baada ya kuchanganya inalowekwa kwa siku mbili, siku ya tatu wanaweka unga wa mchele na kuipika katika pipa kubwa kwa masaa matatu, inakuwa imeiva tayari kwa kunywa. Lita moja Tsh. 400, ubovu wa barabara na kukosa soko la zao la mchele unaolima kwa wingi ndio unasababisha mchele huo tutengeneze pombe ya mpunga kwa kujipatia kipato

“Mazao mengi tunalima lakini hakuna barabara ya uhakika kusafirisha mazao mpaka soko kuu la mazao SODECO Songea, unaweka mpunga ndani mpaka unaliwa na wadudu na kuharibika, ukiwa na mpunga inakubidi utengeneze pombe ya mpunga ili usiharibike,” Alisema Emanuel Komba.
Wanakijiji wa Ifinga wanalima mazao ya chakula na biashara lakini wanakwama kufikisha katika soko la mazao SODECO kwa ubovu wa barabara, mazao hayo kama mtama, ufuta, tangawizi, ndizi, ulezi, uwele, mpunga, maharage na  miwa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Beatrice Msomisi, alikili kuwepo kwa ubovu wa barabara katika kijiji hicho, alisema sio Ifinga tu Vijiji vingi vya Wilaya ya Songea barabara zake ni bovu sana.
Kipindi cha Masika barabara mbalimbali za vijijini hazipitiki kiurahisi kwa sababu ya ubovu, sio mazao tu kuletwa sokoni, hata mgonjwa na kufikisha madawa kwenye Zahanati mbalimbali ni tatizo kubwa.
“Bajeti ninayopewa katika barabara ni ndogo sana napewa Tsh. Milioni 600 kwa mwaka, za kukarabati barabara mbalimbali za vijijini na mjini, pesa ni ndogo sana ukilinganisha na hali halisi ya ubovu wa barabara hizo na ukubwa wake,” alisema Msomisi.
Milioni 600 tunayopewa  kwa ajili ya kukarabati barabara ni ndogo sana ukilinganisha na ubovu wa barabara zenyewe, pesa hiyo ukikarabati barabara kwa kiwango kizuri ikiwa inapitika kipindi cha masika na jua kali unakarabati barabara moja tu. Umbali wakutoka kijijini kwa kutumia gari ni masaa 2 na nusu kwa pikipiki ni masaa 3 hadi 4.
Aidha aliiomba Wizara husika kuwaongezea pesa katika ukarabati wa barabara  mbalimbali   za  Wilaya hiyo, kwa sababu ziko katika hali mbaya sana na kipindi kama cha masika hazipitiki kabisa na kunakuwa hakuna mawasiliano kati ya Vijiji na Wilaya.
Kutoka Ifinga mpaka kufika makao makuu ya Wilaya ya Songea ni kilometa 219, na kilometa 48 ni barabara ya vumbi, Wilaya ya Songea ina ukubwa wa kilometa za mraba 16,000 idadi ya watu kwa sensa ya mwaka huu ni 170,000.
Imeandikwa na  Mariam Mkumbaru January 3rd, 2013.
Ahsante kwa makala hii  labda niingezee kidogo hapa ni kwamba kijiji hicho pia ni hulima machungwa au walikuwa wanalima machungwa na wwalikuwa wakibadilishana machungwa kwa chumvi kama mtu alikwenda huko na chumvi yake. Nasema hivi kwa vile kuna mtu ambaye yupo karibu sana nami alishafanya hivyo. Walifurahi sana kupata chumvi na yote inatokana na kutokuwa na usafiri/barabara nzuri.

No comments:

Post a Comment