Saturday, August 22, 2015

PICHA YA WIKI: AMA KWELI UKITAKA KUPENDEZA LAZIMA MAUMIVU YAWE.....

Huu ni ubunifu mpya ambao mimi sijawahi kuusikia wala kuutumia. Je wewe umewahi? Basi nikutakieni mwisho wa juma mwema. Panapo majaliwa tutaonana tena. Kapulya wenu:-)

5 comments:

  1. Aisee hii imenikumbusha mbali, tumeitumia sana enzi hizo huko kijijini
    pamoja na vibati unatomboa matundu unatia mkaa, ilikuwa hatari kweli

    ReplyDelete
  2. Duh! mie nakumbuka mama alikuwa akitumia kipande cha chungu..kigae ama kweli watu tumetoka mbali. Lakini afadhali hii haina madhara kama tu hutaungua:-)

    ReplyDelete
  3. Sisi tulikuwa tunapaka dawa ambayo ilikuwa inatengenezwa nyumbani.iliitwa ZAA-ZUU.ilikuwa hatar sana ni kama relaxer ya Kiswahili.pia ilikuwa ni RISK kwa sababu haina vipimo na madawa makali walikuwa wanatumia kuitengenezea.ukishamaliza kuweka hiyo dawa unapaka dawa nyingine iliitwa YOMBOO inafanya nywele kuwa nyeusi.
    Basi wakati wa sikukuu weee tunapendezaje sasa.kweli tumetoka mbali sana.

    ReplyDelete
  4. Sorry ni Mama Wane jamani sio WAND.Pia urembo huo nilioelezea hapo juu asili yake ni Kigoma.

    ReplyDelete
  5. Dada yangu Mama Wane! Duh umenikumbusha mbali sana ZAA-ZUU yaani iliwaka moto hiyo... hakika tumetoka mbali....halafu mnakumbuka kuna mti fulani hivi huku kwetu Ruvuma tulikuwa tukiukita mdawa, ulikuwa ukitumika kupiga meno yaani kama vile mswali ni mzizi wake..meno yanakuwa maupe na midomo inakuwa kama ulepaka lipstik.

    ReplyDelete