Wednesday, August 12, 2015

MAISHA NA JAMII:- ZITAMBUE SIFA SITA ZA MSINGI ZA MWANAMKE ALIYE MKE BORA!

Mithali 14:1 "Kila mwanamke aliye na Hekima hujenga nyumba yake,bali aliye mpumbavu
huibomoa kwa mikono yake."

Kuna mithali isemayo "MAJUTO NI MJUKUU", ni kawaida kwa wanandoa kuangalia na
kulaumiana juu ya matatizo yanayojitokeza, badala ya kutafakari chanzo cha matatizo. Matatizo
mengi ya ndoa yanatokana na wanandoa kutokuwa na elimu ya ndoa na kutofuata ushauri wa Mungu
aliyeanzisha Ndoa. Baadhi ya sifa zamwanamke mwenye hekima pia soma mithali 31:10-31.

-Hufumbua kinywachake kwa hekima, na sheria ya wema katika ulimi wake huwashauri wengine kwa ukarimu mithali (31:26). Wanawake wengi hawajui kuutumia ulimi / ukali,maneno ya mikato, matusi, ukaidi n.k. kwao ni mambo ya kawaida wengi wanatawaliwa na HASIRA na WIVU, akiona mumewe anacheka na wanamke ni kosa la jinai, mwanamke anafura wala hata hawezi kuongea, hali ya hewa inabadilika hata paka nyumbani wanatambua kuwa hali ni mbaya.

-Hufanya kazi kwa moyo na huamka alfajiri na mapema.Kuna wanawake ambao ni wavivu
kupindukia, inafika wakati hata kutandika kitanda anamtuma House Girl, wanaume ni rahisi sana
kuvutwa na anayemhudumia kwa ukaibu, House girl akiandaa chakula, mara kitanda, mara maji ya
kuoga, mara apige deki chumbani n.k. Haitachelewa mwanaume kulipa fadhili kwa wema
anaotendewa.

-Ni msafi na anajua kuandaa mavazi yanayofaa kwa familia yake.
Kuna wanawake ambao ni wachafu/ usishangae kukuta sufuria kwenye makochi, chumba cha kulala
ni stoo ya nepi za mkojo na nguo chafu,wengine kuoga ni anasa. Mwanamke ni MAJI, sharti
mwanamke awe msafi muda wote, Wanaume wote wanapenda usafi,marashi hata ya mchina
yasikose,mwanamke hakikisha "Reception" inakuwa safi na kuwa katika hali ya kumfanya mume
ajisikie kujipumzisha kwa raha mustarehe.

-Jali na timiza mahitaji ya NDOA kwa mume wako.
Sulemani anasema mwanamke mwema “Taa yake haizimiki usiku”, kuna wanawake wavivu kwa
swala hili, pia kuna wanaopenda kulipa visasi kwa kuwanyima waume zao huduma, utakuta wiki

nzima mama apanda kitandani huku amevaa “KOMBATI”  utafikiri ni askari anaendavitani. Wanaume
ni sawa na Mbuzi ambao hawachelewi kukata kamba wakikosa majani walipofungwa, Fanya makosa
yote lakiniusijefanya  ujinga wa kumkomoa mume kwa kumnyima huduma ya ndoa,  hilo ni kosa la
jinai. Hakikisha huduma hizo zinaboreshwa, nenda na wakati ili mradi isiwe kinyume na taratibu za
Mungu.

-Mwanamke anatakiwa kujua kupika chakula kitamu, ambacho famiia itafurahi.
wanawake wengi hasa siku hizi hawajui kupika, ndio maana utakuta wanaumewengi wanaishia kula
hotelini au kwa mama ntilie, kama umetokabara basi usione aibu kujifunza kwa watu wa pwani namna ya kuunga nazi kwa chakula. Akina mama ni wajibu wao kujifunza Mapishi, mchicha peke yake unaweza kuwa na mapishi zaidi ya 10, Wanaume wanapenda chakula  chenye ladha “Taste”, mfanye mume akumbuke chakula cha nyumbani.

-Mwamini mume wako, wivu na hisia mbaya ni adui wa ndoa yako. Usitoe siri za ndoa yenu kwa
mashoga au ndugu zako.

Muda wote muombe Mungu akupatie hekima ya kuongea pindi tatizo linapotokea, muombee mume wako ili Mungu amsaidie pia awe na hekima ya kutunza ndoa kwa uadilifu na upendo”.
CHANZO: GAZETI LA MWENGE TOLEO LA JANUARI 2015

No comments:

Post a Comment