MAMA! ANAWEZA KUCHUKUA NAFASI ZA WENGINE LAKINI NAFASI YAKE HAIWEZI KUCHUKULIWA NA YEYOTE YULE
KUZALIWA 2/10/1952-KUFA 17/8/2004
Mama ni miaka kumi na moja sasa tangu ututoke. Umetuacha na majonzi pia maumivu moyoni mwetu. Tunaukumbuka sana uwepo wako, tukiamini Mungu angekuacha japo kwa miaka michache. Midomo yetu haiwezi kuelezea jinsi tulivyokupenda. Lakini Mwenyezi Mungu anajua ni jinsi gani tulivyokupenda. Na jinsi gani tunakukumbuka, mapenzi yako, wema wako. Pia kama mama kwa mwongozo wako katika nyumba yetu, ambayo sasa ni upweke mtupu bila wewe.
Tunakukumbuka sana, sisi wanafamilia wote pamoja na ndugu wote na pia marafiki. KIMWILI HAUPO NASI, BALI KIROHO UPO NASI DAIMA. MWENYEZI MUNGU AIPUMZISHE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI. AMINA!!!
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu mama yetu. Aaaamin
ReplyDeletePoleni sana ndugu zetu na endeleeni kudumisha mioyo iliyojengewa uvumilivu.
ReplyDeleteAhsanteni sana kaka zangu kwa kuwa pamoja nasi kwa siku hiii ya kumbukumbu ya mama yetu.
ReplyDeletePoleni sana na Mungu amrehemu mama yetu.
ReplyDeleteMama Wane! Kwa niaba ya familia ya Mzee Ngonyani nasema ahsante kwa kutufariji.
ReplyDelete