Monday, November 3, 2014

TUANZE JUMATATU HII NA MCHAKAMCHAKA...WIMBO

Unakumbuka wimbo huu....Idi Amin akifa mimi siwezi kulia nitamtupa Kagera awe chakula cha mamba....Au Alisema, Alisema, Alisema Nyerere alisema vijana wangu wote mwalegea sharti muanza mchakamchaka, chinja, au....Je wewe nawe kuna mwimbo wa mchaka mchaka uukumbukao?

4 comments:

  1. Mchaka mchaka chinja!
    Akija kaburu chinja!
    Mchaka mchaka chinja!
    Akija fisadi chinja!
    Mchaka mchaka chinja!
    Akija vijisenti chinja!
    By Salumu.

    ReplyDelete
  2. Kaka Salumu Ahsante kunikumbusha huu wimbo maana ndo uanzapo tu kukimbia lazima uanza na huu...
    Unaukumbua huu;. Mwalimu Nyerere kasema vijana fungeni mikanda....

    ReplyDelete
  3. Habari!
    Wimbo mwingine jua lile litelemke mama aya hiya aya hiya na
    Mbuga za wanayama Tanzania ya kwanza ni Serengeti, Ngorongoro, Manyara na Mikumi oo Tanzania oye

    na Vumilia kidogo huu ulikuwa unaimbwa hasa na wanaokaribia kumaliza darasa la saba maarufu kama LY.

    ReplyDelete
  4. Kaka Salehe huo wimbo wa jua lile litelemke naukumbuka ...Ila hiyo mingine ni migeni kwangu...Ahsante kwa mchango wako:-)

    ReplyDelete