Hii kazi hii ilikuwa kazi ya karibu kila siku maana usipotwanga mihogo hakuna ugali...basi hapo unapomaliza kutwanga uso mzima ni kama vile umemwagiwa unga...Tulikuwa tukipaka usoni kama poda mweeeeee...kaaaazi kwelikweli. Nimekumbuka sana enzi zila na pia nimetamani ugali wa muhogo na kisamvu chake...si unajua hakitupwi kitu maganda ni chakula cha nguruwe mmea mzuri sana huu
Da Yacinta nakubaliana nawe: Ya kale dhahabu japo ukifanya hivyo unaonekana mshamba na anayeturudisha nyuma. Afrika hakuna ma-junk ati. Huo ugali wa muhogo au bada usiambiwe.
ReplyDeleteRaha ya nyumbani,chakula bora,hakuna upweke...
ReplyDeleteAsante Sana Kadala.
Kaka Mhango ..lakini wakati mwingine ni afadhali kuonekana mshamba huku ukijali utamaduni wako
ReplyDeleteKACHIKI! chakula kama hiki ni bara sana ila inasikitisha wengi wameaacha kula ...
Da Yasinta nakubaliana nawe. Huwa sisikilizi anachosema mtu bali unachosema moyo wangu. Ushamba wangu hahumhusu yeyote. Usijali kuonekana mshamba. Maana kuna kipindi anayeweza kukuona wewe mshamba akawa mshamba kuliko wewe na anayekuona mbaya akawa mbaya kuliko wewe. Hivi mtakatifu Kitururu mna mawasiliano? Nilipita ugani kwake nikakuta ametekwa kama ulivyokuwa umefanyiwa.
ReplyDeleteKaka Mhango nimekupata...Mtakatifu nimeona hapa kwake haiwezekani kuingia nitampa taarifa
ReplyDeleteobat telat bulan i think your blog very informative cytotec thanks for sharing obat penggugur
ReplyDelete