Saturday, September 6, 2014

UJUMBE TOKA MAISHA NA MAFANIKIO....

Nimeamka asubuhi hiii.... kama kawaida yangu huwa napitia barua pepe yangu...na leo nimekutana na ujumbe huu nimetumiwa na msomaji wa maisha na mafanikio. nikaona si mbaya nikiweka hapa ni kama ufuatavyo--------- karibu tujadili pamoja

Ni kwamba usipoteze muda  wako kuwa na watu/marafiki ambao hawana muda na wewe, yaani kila siku uwafuate wewe, kila siku ni wewe kuwapigia simu, kila siku ni wewe kuanzisha hadithi. Kama kweli wanakupenda na kukujali kama wasemavyo basi  watakutafuta, kwa vile wanajua wapi unapatikana, huna  haja ya kujipendekeza/kubembeleza, na wewe ni binadamu muhimu vilevile.
NAPENDA KUWATAKIENI WOTE JUMAMOSI NJEMA. TUPO PAMOJA

4 comments:

  1. Ujumbe mzito kweli kweli. Mie huwa sipendi wanaonitafuta kunipiga bomu. Hivyo kutafutwa au kupigiwa simu na watu si kigezo cha kukupenda wala kukuthamini. Huwa nachukia ujumbe wa "Tafadhali nipigie". Kama una shida si utwange wewe na uronge?

    ReplyDelete
  2. Ni kweli ujumbe mzito...mimi huwa nasema rafiki ni wakati wA shida na raha.......huo ndio urafi/ undugu bora.

    ReplyDelete
  3. Ujumbe mzuri kwa mtu ambaye hajiamini. mtu kuto nipigia simu,au kunitafuta kwa mawasiliano yeyote yale sina hakika kama si rafiki mwema au hanipendi? ninacho angalia mimi katika maisha ni kwamara ya mwisho rafiki huyo mliachana vip kwaubaya ama kwa uzuri,basi .kwa hiyo hata ikichukua miaka hatuja wasiliana tukionana tunaendeleza pale tulipa ishia . hii ya kujuwa na kwenye tabu na raha sioni kama ni kikwazo katika urafiki wa mtu namtu. ukitokea kwenyeshida safi,pia usipotokea sitajuwa ukotika hali gani yaani nini kimekusibu. . kaka s

    ReplyDelete
  4. Ujumbe mzito na mzuri sana Dada yangu,binafsi umenifunza inabidi nianze kubadilika kidogo,Nawatakia wiki njema

    ReplyDelete