Tuesday, September 16, 2014

NIMEKUMBUKA SANA KWETU LUNDO/NYASA

 
Hapa ni samaki wapo kwenye mtungo ndo wanatoka tu kuvuliwa...nadhani ni vituhi, ukipata na ugali wa muhogo hapo halafu na tembele au kisamvu eeeehhh bwana we basi tu. Haya kila la kheri kwa wote!!!

10 comments:

  1. Yaani usiniambia nami nilivyowatamani...

    ReplyDelete
  2. samaki wa nyumbani tz niwatamu sana hasa uwapate wakiwa wabichi.maziwa namito yetu inatupa samaki safi kabisa. mi nikiwa tz samaki ndo kipaombele katika siku ambazo niko tz. Nina mkakati wa kuwa natembelea sehemu ambazo samaki wanapatikana wakiwa wabichi nakupikwa hapohapo.kaka s

    ReplyDelete
  3. Kaka S...sio wewe tu tupo wengi twafanya wengi...samaki ni watamu kwa kweli wa kupika, kukaanga na kuchoma

    ReplyDelete
  4. Mtu kwao, mzarau kwao ni mtumwa au sio ndugu wangu

    ReplyDelete
  5. Da Yacinta njoo Kanada utawakimbia. Pamoja na kuwa mbali nawala karibu kila jumamosi ukiachia mbali kuku wa kienyeji ambao huku wao huwaita hard chickens for soup. Tofauti ni kwamba nawapata wakiwa wamegandishwa ambapo nyumbani unawapata toka jikoni kwa Mungu. Pia huwa inakuwa vigumu kupata ile ladha ya asili na shombo lenyewe. Hata hivyo, umenikumbusha nyumbani.

    ReplyDelete
  6. emu-three! Yaani haswaa mtu kwao!!

    Kaka Mhango...Usiombe nije Kanada maana itakuwa kila siku ni samaki tu..Maana kama kweli mtu una nia na unapenda hizo/hicho chakula wala si mbali ila mifuko itatoboka:-)
    Kamala! Nilikumissije ndugu yangu karibu sana hapa kwetu. Niko Mbioni kwenda na nitawala ww acha tu....

    ReplyDelete
  7. Kamala ni furaha kusikia hilo kuwa umerudi rasmi....muda wa kwenda kula samaki ukikaribia utajua-:)

    ReplyDelete