Friday, September 19, 2014

KWA NINI SALOMON ALIKUWA NA WAKE 700?/Why Solomon had 700 wives?

 
Katika matembezi yangu nimekutana na habari hii, nimeipata Jamii Forum. Haya karibu......

Juzi nilipokwenda dukani kununua liwa kwa ajili yakurembesha uso wangu. Muuzaji alinifungia liwa hiyo kwenye kipande cha karatasi ambacho kilikuwa na habari inayomhusu Nabii Suleiman AS.Huyu nabii anaelezwa kwamba alikuwa na utajiri mkubwa usiyo kifani, lakini pia alikuwa na busara na hekima haijapata kutokea hapa duniani. Alikuwa na nguvu sana na utajiri wake ulikuwa ni mkubwa usioweza kupimika.Lakini pamoja na kujaaliwa neema zote hizo lakini vyote hivyo havikuwa na maana yoyote kwake.
Inasemekana alikuwa ni mwanaume shababi mwenye siha nzuri. Pamoja na kuwa na wake 700 na nyumba ndogo zipatazo 300, lakini kamwe hakuna na amani moyoni mwake.
Je ni kitu gani alikosa nabii huyu?
1. Wake warembo alikuwa nao 700
2. Nyumba ndogo zilizojaaliwa neema za Allah zilikuwa
3. Hekalu kubwa lenye kila aina ya nakshi vikiwemo vito vya thamani
4. Utajiri mkubwa usio na mfano ulikuwa mikononi mwake
Alikuwa ana uwezo wa kupata starehe zote alizozitaka hapa duniani zikiwepo pombe za kila aina huku akiwa amezungukwa na wanawake warembo wa kila sampuli waliojaaliwa neema za Allah……. Mh!
Unaweza kushangaa, Je ni kitu gani amekikosa mtu huyu?

Naam, hebu angalia maisha ya vijana wa kiume wa nyakati hizi.
Wanahangaika sana kutafuta fedha, wanajenga mahekalu,wananunua magari ya kifahari, wanaoa wake warembo, wanakuwa na uwezo wa kula starehe sana tena za kila aina, watatafuta nyumba ndogo zisizo na hesabu,lakini bado hawatatosheka.

Pamoja na habari hiyo ya nabii Suleiman ambayo wengi wetu tunaifahamu vyema, lakini bado vijana wa kiume wameshindwa kung’amua kwamba hivi vitu vya nje, yaani Fedha, na fahari zote za dunia si chochote, na kamwe haviwezi kutuletea amani na ridhiko hata siku moja katika maisha yetu.


Kama Nabii Suleiman hakupata ridhiko kwa amali alizojaaliwa na Mwenyenzi Mungu seuze wao!


Ni kuhangaika tu kusiko na mashiko na kamwe fedha,mahekalu na wanawake wanene wanene wenye makalio makubwa na matiti yenye kututumka vifuani na sura za kuvutia si mali kitu, havitawafaa hata kwa miaka dahari.

Mtafuteni Mungu atawaongoza, acheni michepuko,tulieni na wake zetu.
NACHUKUA NAFASI HII NA KUWATAKIENI MWISHO MWEMA WA WIKI....KAPULYA

6 comments:

  1. Da Yasinta umenikosha kwenye para ya mwisho.Yaani wanene wenye...... na kututumka...hehehe! By Salumu.

    ReplyDelete


  2. Habari!
    Asante kwa ujumbe murua, nyongeza tunachokitafuta pamoja na mungu ni ridhiko la moyo
    ambalo halitoki nje yetu bali ndani mwetu kwa maana katika kuamini katika sisi na kuwa furaha amani na ridhiko la kweli ni uamuzi wako mwenyewe na si nje yako. Ukweli huu unatusumbua wengi na kwa bahati mbaya wengi hatujui kuhusu hilo hata kama tunajua tunajitoa akili.
    Kila la kheri na Jmosi njema.










    ReplyDelete
  3. Kaka Salum! Ahsante kwa kupita hapa na kuacha lako lililo moyoni

    Kaka Salehe ahsante sana kwa mchango wako katika kibaraza hiki. Jumamosi iwe njema kwako pia.

    ReplyDelete
  4. Hakuna kitu kama hicho. Ni hadithi za Pwagu na Pwaguzi zilizopewa uhalali kwa kuingizwa kwa kivuli cha dini. Mtu wa Mungu hawezi kuwa mzinzi kiasi hiki halafu unaambiwa alikuwa na hekima hakuna duniani. Angekuwa na hekima angeogopa uzinzi. Kama alikuwa na hekima basi ni ya kimwili. Kiroho alikuwa mtupu na mdhambi mkubwa tu.

    ReplyDelete
  5. kweli kabisa kwani kuishi kwa kumtumainia MWENYEZI MUNGU kunafaida saana

    ReplyDelete
  6. Kaka Mhango...naweza kukubaliana nawe kwa kiasi fulani kwa kweli wake wote hao wa nini jamani mmoja tu mtu anafikiri vipi kumtunza....
    Veronika! Kwanza napenda kukukarisha sana hapa kibarazani pia ahsante kwa mchango wako.

    ReplyDelete