Samahani kuadimika ila nipo kiaina ....
..Nipo likizo na nilikuwa nimejificha hapa na kublog ilikuwa ni kaziii kwelikweli. Nilikuwa na wakati mzuri sana na familia pia baadhi ya marafiki. katika picha hapo unaona kitu fulani ni wanetu wapo ziwani kuvua samaki...baada ya muda wakarudi na samaki......Na ndo ikawa kazi yangu kumtoa samaki magamba. Kwa vile nimekulia samaki hakuwa kazi kubwa na ngungu kwangu.:-)
Da Yasinta tumekumisi sana! Hivi hilo ni ziwa Tanganyika? Tufundishe unavyochoma samaki. By Salumu.
ReplyDeleteKaka Salumu....ahsante nami nimewamiss mno. Hapana si ziwa Tanganyika...kuchoma samaki...ukisha mtoa magamba..unaweka viungo uvitakavyo na halafu kuchoma...usisahsu pilipili
ReplyDeleteHongera kwa likizo
ReplyDeleteKila la kheri na likizo njema
Kaka Salehe! Ahsante nawe uwe na siku njema
ReplyDeleteLikizo njema Dada Yasinta
ReplyDeleteAhsante dada Manka ....njoo tule ugali na mchicha , figiri na mboga maboga-:)
ReplyDeleteDada yangu unanitamanisha natamani ningekuwa karibu,asante sana,jumapili njema
ReplyDelete