Saturday, May 10, 2014

TAHADHARI :UGOMVI UNAATHIRI AFYA YAKO!!!


 
Wanaume wasio na ajira wako katika hatari ya kuathirika zaidi kutokana na ugomvi
 
Ugomvi wa mara kwa mara baina ya wapenzi, marafiki ama hata jamii unaongeza hatari ya kufa kwa watu wenye umri wa makamo. Haya ni kwa mujibu wa watafiti nchini Denmark.
Watafiti wamesema kuwa wanaume na wale ambao hawana kazi wako katika hatari Zaidi.
 
Utafiti huo katika jarida la 'Epidemiology and Community Health', unasema kuwa shughuli za kukidhi matakwa na mahitaji ya jamii pia zimehusishwa na idadi kubwa ya vifo vya mapema.
Pia kulingana na utafiti huo utu wa mtu na uwezo wa mtu binafsi kukabiliana na dhiki ilichangia katika matokeo ya utafiti huo.
Ingawa watafiti hao kutoka chuo kikuu cha Copenhagen waliweza kupata uhusiano uliopo kati ya vifo vya mapema na kugombana, na kuwa ugomvi uliongeza hatari ya vifo vya mapema mara tatu, hawakuweza kuelezea kikamilifu sababu haswa ya hali hiyo.
Utafiti wa hapo awali ulionyesha kuwa watu wenye wasiwasi mwingi na mahitaji mengi kutoka kwa wapenzi wao na watoto, pamoja na wale wanao gombana mara kwa mara na jamaa wao, wamo katika hatari kubwa zaidi ya kuugua magonjwa ya moyo na kiharusi.
Tafiti za hapo awali pia zaonyesha kuwa utangamano mwema na watu pamoja na marafiki wengi ina athari chanya katika afya, huku utu kwa kiasi kikubwa ukiamua jinsi mtu hupokea na kuguswa na hali za kijamii pamoja na mahusiano.

Wapendanao hawapaswi kugombana

Kumsumbua mpenzi wako pia kunahatarisha afya
Katika utafiti huu, watafiti walisema kuwa athari za kisaikolojia zinazosababishwa na dhiki, kama vile shinikizo la damu na ongezeko la athari ya magonjwa ya moyo, ndizo hasa zinaweza kueleza athari ya ongezeko la vifo vya mapema.
Utafiti umeonyesha kuwa wanaume wanapokabiliwa na hali za dhiki kwa kuongeza homoni inayokabiliana na hali ya dhiki na wasiwasi, jambo ambalo linazidisha athari ya kiafya.
Utafiti huo ulihusisha watu 9,875 wake kwa waume wenye umri wa kati ya miaka 36 na 52 na ulitumiwa kuchunguza uhusiano uliopo baina ya hali ngumu ya uhusiano wa kijamii na vifo vya mapema.
Wote walikuwa wameshiriki katika Utafiti ‘Denmark Longitudinal’ kuhusu Ajira, ukosefu wa ajira na afya , kuanzia mwaka wa 2000.
Utafiti uligundua kuwa wasiwasi wa mara kwa mara au mahitaji yanayotokana na wapenzi na watoto ulihusishwa na ongezeko la kufikia 50%- 100% la vifo vya mapema.
Ukosefu wa ajira ulionekana kuongeza athari hasi za uhusiano mgumu wa kijamii. Wale ambao hawako kazini wameonekana kuwa katika hatari kubwa zaidi ya kifo kutokana na jambo lolote kinyume na wale walio na kazi.
wanaume pia wako katika hatari zaidi kutokana na mahitaji na wasiwasi unaotokana na wapenzi wao wa kike , huku wakiwa katika hatari kubwa zaidi ya kifo zaidi ya ile ambayo kwa kawaida imehusishwa na kuwa mwanamume.
Dakta Rikke Lund, wa kitengo cha afya ya umma katika chuo kikuu cha Copenhagen amesema kuwa wasiwasi na ugomvi ni sehemu ya maisha. Lakini akaongeza kuwa watu ambao wanakuwa na migogoro mara kwa mara wako katika hatari zaidi lakini wanaweza wakasaidiwa.
CHANZO: BBC.

1 comment:

  1. Ni tafiti nzuri sana na ni kweli kabisa hasa kwa wenzetu nje ambao majukumu mengi ni kwa babab. Ila tafiti kama hii ingefanyika Tz majibu yangekuwa opposite kwani wanawake wengi ndio waathirika wa hayo magonjwa na ndio wanawajibu mkbwa kwa familia wakati wanaume wengi waki Tz wanaishia kunywa mapombe na kutafuta wanawake wa ziada na pia hawajali familia kabisa! Kwetu tz jukumu kubwa la familia ni kwa mama na maginjwa hayo kwa kina mama ni wengi kuliko wanaume. Mungu atusaidie ili tafiti kama hizo ziweze kufanyika na kwetu pia. Naongezea tu Mungu aiepushe Tz yetu na dengu fever.

    ReplyDelete