Nimeona usipite muda zaidi bila kuzikumbuka METHALI zetu basi ungana nami katika hizi chache nilizozikumbuka leo:-
1. Aninyimaye mbaazi, kanipunguzua mashuzi
2. Biashara haigombi.
3. Chanda chema huvikwa pete.
4. Dua la kuku halimpati mwewe.
5. Fimbo ya mbali haiui nyoka.
6. Kikulacho ki nguoni mwako.
7. Kosa moja haliachi mke.
8. Lisilokuwepo moyoni halipo machoni.
9. Mapenzi ni kikohozi hayaweza kufichika.
10. Mficha uchi hazai.
BLOG YA MAISHA NA MAFANIKIO INAWATAKIENI WOTE SIKU NJEMA SANA NA WOTE MNAPENDWA:-)
mtaka cha uvunguni, sharti ainame
ReplyDeleteasante dada kutukumbusha
Hiyo nayo ni nzuri. Ahsante. Elimu hawanyimani!
ReplyDelete