1. Maua mazuri yapendeza x 2
Ukiyatazama utachekelea
Hakuna mmoja asiyeyapenda x 2
Kwa kutaka kuimba bila kukosea basi fuata hii hapa:-)
Au pia tusiwasahau na watoto, si mnakumbuka na huu wimbo haya wazazi waimbieni watoto wenu kwa raha zote ni kama vile umsomeapo/msimuliapo hadithi :-
2.Mtoto msafi apendeza x 2
Ukimtazama utachekelea
Hakuna mmoja asiyependeza x 2
3. Mtoto mtii apendeza x 2
Ukimtazama utachekelea
Hakuna mmoja asiyempenda x 2
JUMAMOSI IWE YENYE UPENDO, FURAHA JUU YA KICHEKO. SI MNAJUA KUCHEKA/KICHEKO NI DAWA ISIYOLETA MADHARA.
KUMBUKENI TUPO PAMOJA!!
Nimeipenda post ya leo, mauaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa.
ReplyDeleteAhsanteeeeeeeeee....mimi pia ni mpenzi mno wa maua
ReplyDeleteNimependa sana rangi ya hilo ua,umenikumbusha mbali sana na hizo nyimbo,weekend njema Dada yangu
ReplyDeleteDada Manka....yaani hata mie hiyo rangi nimeipenda si kawaida ua la bluu. Ni furaha kwangukana umepata kumbukumbu.....naamini nawe utakuwa na weekend njema.
ReplyDeletejamani rafiki umenikumbusha mama yangu (may her soul rest in peace) alikua anapenda sana maua, its a shame sisi watoto wake hakuna aliyerithi hili la upenzi wa maua...
ReplyDeleteMimi nimekua kwenye mazingira ya kuzungukwa na maua si ndani wala nje ya nyumba, vurugu tupu! Tukisafiri airudi huko lazima amebeba ua jipya!
nimesahau kuweka jina hapo juu, ila ni mimi rafikio....
ReplyDeleteRafiki yangu....si watoto wate hywa wanarithi wazazi walivyo. Huna haja ya kuona aibu inawezekana umerithi kitu kingine. Mama anakuelewa.
ReplyDeletenakubaliana na wewe rafiki
ReplyDelete