Asubuhi ya leo nimeamka huku nikiwa na hamu ya chakula hiki cha asubuhi. Maana huu ndio msimu wake hasa kwetu Songea maana ndio msimu wa mvua....mmmmhhh....halafu nikakumbuka ....
..mahindi jinsi mtu aendavyo tu shambani kukata/kuvunja mahindi na kwendajikono kuchoma au kuchemsha pamoja na maboga wakati huko nje mvua inanyesha..Ahhh nausikia utamu wake. Halafu nina kahadithi kamoja kuhusu mahindi tulikuwa tunaitumia sana tulipokuwa wadogo inakwenda hivi:- Kila mtu anakuwa na muhindi, sasa wale wadogo huwa hawawezi kula basi wakubwa walikuwa wakiwaambia leta mimi nikutengenezee barabara ya kwenda ....anataja mji. Sasa yule mdogo aelewi anampa kumbe mwenzake yale mahindi atengenezayo barabara yote yanaingea tumboni ...Utoto bwana. Nilijaribu siku moja na wanangu, nilifanikiwa:-)...mmmhh ngoja niache niwahi Madaba/matetereke...maana ndiko nilikojifunza/onja mara ya kwanza Magimbi. Kwa hiyo leo nimekaa na kuota vyakula vingi. Natamani magimbi haya yawe mlo wangu wa mchana huu. Je kuna mlo ambao na wewe unautamani/hujala muda mrefu?
Umewahi kula mawungu?
ReplyDeleteUsiye na jina ..Halafu nahisi kama vile wewe ni mngoni:-) Mavungu nimewahi kuyaona na nayajua ila sijawahi kula kwa kweli..ila kwa hisia zangu nahisi yananoga kama kumbukumbu vile:-)
ReplyDeleteNatamani senene, lakini samaki nchanga simtaki. By Salumu.
ReplyDeleteKaka Salumu ...kwelu humtaki samaki nchanga? Na sato je?
ReplyDeleteYasinta samaki nchanga unanjua? kama humjui basi ni panya waleee ulioweka kama mboga siku moja hapa na ugali!!!!!!sijui nimepatia kaka Salum?
ReplyDeleteOh...kumbe. duh, hizi lugha hizi...basi twende huko kwenye senene kaka Salumu au pia kama likungu lipo
ReplyDeleteUmepatia. Samaki nchanga ni yule panya alokuwa kwenye ugali katika picha moja iliyowekwa hapa! Sato wa MZA ni wanono mno! By Salumu.
ReplyDelete