Thursday, March 6, 2014

TUSISAHAU TULIKOTOKA:- UDONGO NA MANUFAA YAKE......

Lengo kuu zaidi la kuweka vifaa hivi vya asili ni kutaka kumjibu ndugu yangu KACHIKI katika mada yake kuhusu mitungi/vyungu. na je kwa lugha yangu vipi tunaita?
Chungu kikubwa kidogo ambacho kama familia ni kubwa waweza kupikia chakula kushiba kama vile Makande, au kitoweo:-) Au pengine hata kuwekea maji ya kunywa kama nifanyavyo mimi hapa:
Na hapa ni vyungu vya kawaida kwa kupikia mboga. Nakumbuka hapo zamani vyungu vilitumika kupikia kila na vyakula vyake vilikuwa vitangu sana kwa kweli. Kuna ule utamu wake wa asili ambao ni vigumu kuuelezea ..si kama kupika mboga ,maharagwe, na nyama kwenye sufuria
Undongo wa mfinyazi unaweza kutumika kwa kutengeneza vitu vingi sana ..hapa ni vyombo mbalimbali ..hicho kibakuli ni kwa ajili ya kuwekea sukari au mimi nafanya hivyo..na hivyo vingine ni mapambo tu unaweza kuwekea maua au kuweka kama vilivyo.
Kachiki NAJIBU SWALI LAKO ni kwamba ninavyo kote kote na vilifika salama kabisa kama uonavyo katika picha.  Vyungu kwa KINGONI twaita CHIVIGA na mtungi CHIHULU/CHIFULU. NAPENDA KUWATAKIENI WOTE ALHAMIS NJEMA SANA PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA:-)

3 comments:

  1. Ohhhh..dada wa mimi Yasinta/"KADALA" USENGWILIII...sijui kama nimepatia.

    Yaani kweli wewe ni mwanamke/Mama/Dada Mkuu....

    Hongera sana sana..

    Nikija tutapikia Vyungu tuu mpaka naondoka na Maji ya Kunywa ya Mtungini.

    Yaani unavyo vya kutosha,Mpaka nakuonea WIVU!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Kachiki...ahsante. wala usikonde ututatumia vyungu tuuuu..labda utarudi bacho kimoja.:-D

    ReplyDelete
  3. Duuhh itakuwa Vyema KADALA wa Mimi..

    ReplyDelete