Nimejikuta ghafla kama ndo mimi na mama tukitoka shambani kupanda mbegu za mahindi au mpunga na tunaporudi tumeokota na kuni. Maana kifuku hiki sasa bila kuni hakuna huwezi kutoa chakula kilichoiva ...Duh! nimekumbuka sana enzi zile...Je? wewe unakumbuka kazi gani ulikuwa unaifanya sana au ulikuwa hupendi kuifanya:-)....NAWATAKIENI WOTE IJUMAA NJMA NA PIA MWANZO MWEMA SANA WA JUMA KWA UJUMLA...KAPULYA.
Da kweli kiafrika zaidi yaani.
ReplyDeleteKaka Nicky! Ni haswaaaa kunyumba:-D
ReplyDeleteHata kama umekumbuka kipindi cha kupanda mahindi na mpunga, sina hakika kama hiki kilikuwa kipindi cha kupanda kwa sababu inaonekana kulikuwa kukavu sana. Angalia hayo majani. Mwalimu wangu wa Jiografia alinifundisha kusoma mazingira ya picha. Mimi kwa picha hii nakumbuka wakati wa kuvuna mahindi.
ReplyDeleteKaka Yangu Mhagama..Niliposema hivyo nilikuwa naamanisha kwamba ni kama vile ule wakati wa kifuku yaani hapo katika picha unaona tumebeba kuni kichwani na ndoo mkononi ni kama vile watu wanatoka kupanda mbegu au labda kutia mbolea...Hii ndio ilikuwa maana yangu. Ni kweli kabisa ulivyosema kwamba hapo katika picha inaonekana ni kiangazi...
ReplyDelete