Thursday, February 6, 2014

HII KWA KWELI ITAKUWA PICHA YA WIKI...UGALI KWA NYAMA PANYA !!!MMMMHHH KAZI IPO!!!

Ni muda mrefu nimekuwa nikisikia ya kwamba nyama ya panya na nyoka ni tamu kama ya kuku. Na pia nimesikia katika habari ya kwamba baaada ya miaka wadudu wote watakuwa kitowoe kizuri sana kwa binaadamu. Swali moja kutoka kwa kijana wangu linaulizwa hivi:- Iweje tule panya wakati anatuletea magonjwa? Na je nyoka si adui yetu na pia ana sumu?

8 comments:

  1. Da Yacinta unashangaa hiyo? Nenda Ntwara mkoa wa jirani au Nchumbiji hata Malawi utaona hii kitu inavyoliwa. Malawi inaitwa mbewa hadi watu huigombea. Ukita kuona vizuri nenda youtube ufungue link hiihttp://www.youtube.com/watch?v=WXH9LEhziMc
    Nyoka naye mbona kama samaki. Kwa ufupi dunia yetu ina mambo tofauti sana. Ukishuka pale Zambia viwavi (Catepillar) ni kitoeo kizuri kama senene kwa wajomba zetu wa Kagera, Rwanda, Uganda na DRC.

    ReplyDelete
  2. Mwal. Mgango...hakika duniani mambo tofauti sana ...lakini afadhali wangemtoa hayo manyonya/ngozi......halafu umenikumbusha hilo neno mbewa....wangoni tunasemaga hivyo pia.....hapo mie ntakula hiyo sukumawiki tu....

    ReplyDelete
  3. Lol. Ukila sukuma wiki bado utakunywa mchuzi wa mbewa. Najua wangoni na wanyasa si wale wale toka Sauzi zamani. Umeona mbewa anavyotaka kuvunja ndoa kwenye link niliyokutumia?

    ReplyDelete
  4. Duh jamani panya. Hata hivyo chakula ni chakula ilimradi hakimdhuru mtu afya@nicky mwangoka

    ReplyDelete
  5. Ulivyosema angalau wangempamba kidogo, mie hata hilo sukumawiki kwenye hilo sahani singeliguza... mwanao ana maswali mhimu, vyakula hivi vina faidha gani kwenye miili isopkuwa shibe?

    ReplyDelete
  6. Mwal Mhango najua basi sitakula kabisa hiyo sukumawiki:-) Ni kweli wanyansa na wangoni hatujaachana sana ....walongeza bwaji....ntaangalia hiyo link ninaumwa kakangu.

    Kaka mwangoka! mmhhh!!
    Selina! wasema kweli ndugu yangu

    ReplyDelete
  7. Ndalojenza bwino zikomo kwa mbiri. Uli bwanji bwenzi langa? Ambvuye akudalitse.
    Zikomo chembere.

    ReplyDelete
  8. Mmmhh kaka Mhango! naona hapa lazima narudie kozi maana nimesahau ile mbaya ..maana ilikuwa zamani kweli ...na hii mwauka bwanji..Kwa vile ni mwl.. basi naona haitakuwa shida:-)

    ReplyDelete