1. Asiyekuwepo machoni, na moyoni hayupo.
2. Bendera hufuata upepo.
3. Chururu- si ndo, ndo, ndo.
4. Dua tupu haliachi kuvuma.
5. Fuata nyuki ule asali.
6. Hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe
7. Heri kufa macho kuliko kufa moyo.
8. Ikiwa hujui kufa, tazama kaburi,
9. Jogoo la shamba haliwiki mjini.
10. Kimya kingi kina mshindo mkuu.
SIKU YAKO IWE NJEMA SANA NAWE KAMA UNA METHALI UIKUMBUKAYO KARIBU KUISEMA/ANDIKA.
Malizia methali hizi:
ReplyDelete1. Simba mwenda kimya............
Mhindi alijibu: Simba mwenda kimya iko gonjwa kama siyo gonjwa kanisi!
2. Usipoziba ufa...................
Mhindi alijibu: Usioziba ufa miji tachungulia dani!
3. Fuata nyuki ule...............
Mhindi alijibu: Fuata nyuki ule asali, usifuate nzi utakula m#*i
By Salumu.
Yasome haya yatakusaidia katika maisha yako
ReplyDeleteMueke chura kwenye kiti cha dhahabu utamuona ataruka aende kwenye tope hivi ndio baadhi ya watu walivyo, namna utakavyomuenua atarudi mahala anapotoka....
Usimhuzunikie mtu aliyekubadilikia ghafla, huenda ikawa ameacha kujifanyisha.. (pretend)
Mwenyezi Mungu amewaumba malaika wana akili bila ya matamanio, na akawaumba wanyama wana matamanio bila akili, na akamuumba mwanadamu akampa akili na matamanio, basi ambaye akili yake itashinda matamanio yake anaungana na malaika, na ambaye matamanio yake yatashinda akili yake anaungana na wanyama.
Mwanadamu maishani ni kama kalamu (pencil), anachongwa na makosa ili aandike kwa khati nzuri..anaendelea hivi mpaka kalamu iishe na kunabaki mazuri aloyaandika.
Usililie kila kitu kilichopita na iwe ni funzo kwako, hakuna kitu kinakufanya mkubwa isipokuwa maumivu makubwa, na sio kila kuanguka ndio mwisho kwani kuanguka kwa mvua ni mwanzo mwema.
Uslubu wako ni fani: kutangamana na wengine ndio cheo chako, kila uslubu wako ukipanda cheo chako kinapanda.
Wanamsifu mbwa mwitu naye ni hatari kwao, na wanamdharau mbwa naye ni mlinzi wao...watu wengi wanawadharau wanaowahudumia na wanawaheshimu wenye kuwadharau.
Kuwa na mnyama rafiki ni bora kuliko kuwa na rafiki mnyama!!
Nilitabasamu nilipokosa ninachokitaka nikafahamu kuwa Mungu anataka nipate zaidi ya ninachotaka nikatabasamu tena upya...
Ukiumia kwa maumivu ya mwengine basi wewe ni mwema, na ukishiriki katika matibabu yake, basi wewe ni mtukufu...By Salumu.
Source:Jamii Forum.
DADA NAAMINI KISWAHILI UNAJUA INA INATOKEA KWANZA UNACHAPIA SANA KWAMETHALI ZAKO PILI UNACHANGAYA MISEMO NA METHALI TAFUTA KITABU CHA KIDATO CHA PILI CHA KISWAHILI KITA KUONGOZA KUJUA TOFAUTI KWANI HUWA INACHANGA NYA SANA
ReplyDeleteKaka Salumu ....ahsante. Duh Mhindi alitafuta majibu yake ila mimi ngejibu hivi:-
ReplyDeleteHiyo ya kwanza ni ...ndiye mla nyama
ya pili....utajenga ukuta
ya tatu ....ule asali.
Na pila asante kwa haya maoni mengine ni kweli yatanisaidia.
Usiye na jina wa 10:28AM
Nawe ahsante kwa ushauri nitafanya hivyo.:-)
Kila kuendako hisani hakurudi nuksani bali shukrani.
ReplyDeleteKaka Ray! Karibu sana tena hapa kibarazani kwetu ...Ni kweli shukrani ni muhimu sana ..AHSANTE!!
ReplyDeletevimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg
ReplyDelete