Tuesday, January 21, 2014

MAISHA:- USAFIRI/USAFIRISHAJI KWA NJIA YA BAISKELI...HUPUNGUZA GHARAMA NA PIA MTUMIAJI HUWA NA AFYA NJEMA PIA NI SAFI KWA MAZINGIRA!!!

 Katika maisha usikaa tu na kungoja ..lazima kujishughulisha. Hapa kijana yupo safirini kuelekea soko la kuuza ulazi ila kujipatia kitoweo/chakula. Baiskel zinasaidia sana miaka hii tafauti na miaka tuliokulia wengine kila kitu ilikuwa na kichwani....
 Na hapa anasafirisha chakula, Ndizi hizo..
Naye huyu anaelekea sokonoi kuuza mananasi yake
Na hapa ni baiskel yangu. Kwa kweli usafiri wa baiskel ni mzuri sana na wa haraka huhitaji kusubiri foleni. SWALI:- Umegendua nini kati ya baiskel hizi nne?....Nawatakia JUMANNE NJEMA SANA WOTE

6 comments:

  1. Tena ni mazoezi mazuriii.....hizi picha nimezipenda mnooo

    ReplyDelete
  2. Baiskeli yako nzuri sana. Hivi unaweza kuiendesha kwenye barafu! By Salumu.

    ReplyDelete
  3. Ester...basi mie na baiskel sana... :-D

    Kaka Salumu ...ahsante...kama ni si barafu nyungi naendesha...

    ReplyDelete
  4. hongera kwa kuwa na baiskeli, mie naona baiskeli yako ina kijikapu mbele cha kuwekea mizigo, na hizo 3 hazina. Safari njema uendako na baiskeli yako. Ntakuja unifundishe.

    ReplyDelete
  5. Da Yacinta hayo mananasi dada! Natamani yangekuwa yanakopika na kuwa ya kweli nijichane. Kweli kwetu kuzuri!

    ReplyDelete
  6. Usiye na jina! kwanza ahsante...ni kweli baiskeli yangu ina kikapu mbele kwa ajili ya kuwekea mizigo midogomidogo. Kingine ni kwamba baiskeli 3 zinaelekea upande mmoja kasoro hiyo iliyobeba ndizi. ww njoo nitakufundisha wala usiwe na shaka.

    Mwal. Mhango... si wewe tu hata mimi mate yanavuja ttu hapa ..sijui niyafuate yangu Ruhuwiko?...Kwetu kuzuri sana kakangu...

    ReplyDelete