Wednesday, January 22, 2014

JUMATANO YA LEO TUANGALIE:- JAMII YA KI-SUKUMA!!!

Nimefanya utafiti kidogo kuhusu ndugu zetu wasukuma..nimefanya hivi kwa vile nilipokuwa mdogo nilisimuliwa mambo mengi sana kuhusu wasukuma na babu  yangu mzaa mama pia bibi ..ni Kwamba babu yangu alikuwa fundi mwashi miaka ya hiyooooo......Na hivi ndivyo nilivyopata kuhusu Wasukuma/wanyamwezi...Karibu.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
KWANZA TUANGALIE MAANA YA NENO WASUKUMA:-
Wasukuma ni mkusanyiko wa makundi madodomadogo kutoka maeneo jirani, na kwamba kundi kubwa zaidi limetoka kusini wa eneo hilo la mkoa wa Mwanza. Jina hili limetokana na neno SUKUMA maana yake kwa lugha ya Kisukuma na Kinyamwezi KASKAZINI, yaani moja wapo wa pande nne za dunia yetu. Wanyamwezi ambao lugha yao inafanana sana na Kisukuma huwaita walio Kaskazini mwao "Bhasukuma" yaani watu wa KASKAZINI. Na wasukuma huwaita "Bhadakama" yaani watu wa KUSINI. Siku zote, wasukuma na wanyamwezi walijulikana kuwa wao ni "Bhantu" na kutokana na neno hilo kumekuja kujulikana kundi linaitwa WABANTU. Kundi hili mara zote limetambulika kwa lugha wanayozungumza ya KIBANTU. Hivyo, Wanyamwezi, Wakimbu hadi Wabemba walioko Zambia ni kundi kubwa la wabantu kufuatilia lugha wanazozungumza.
Karibu kujadili nami kama kuna kitu nimekikosa au sahau......JUMATANO IWE NJEMA...

7 comments:

  1. Mwangaloka mayo, ulemhala? Wabheja gutogwa. By Salumu

    ReplyDelete
  2. Sasa wewe yasinta unataka kuwajuwa kwa undani baba zako.wanyamwezi/wasukuma! usijali utafiti mzuri. makabila haya mawili kwa hakika yana hadithi ndefu.nitaongela wanyamwezi kidogo kwani nahusika nao.chimbuko ama asili ya wanyamwezi kwa tanzania ni kabila moja liitwalo WAKONONGO kabila hii ndiyo wanyamwezi asilia napia wanaingiliana na kabila la wakimbu kiasifulani kiasili.wanyamwezi nineno tu lililo patikana katika kuelezea nchi na wapi watu hawa wanatoka.Tabora nimkusanyiko wa makabila mengi,mfano wanyanyembe ,watusi,nk mnyanyembe si myamwezi wa asili.ila kutokana na kuhamahama wengi wamejikuta katia nchi ya wanyamwezi na kuwa wanyamwezi lakini ukifuatilia sana wengi hawana asili ya tabora/ntowola.kaka s

    ReplyDelete
  3. mwangaloka nawe pia..kaka SALUMU..
    hiyo gutogwa ni tongwa au?
    Kaka Sam ahsante kwa historia fupi ya Wanyamwezi/Wasukuma....

    ReplyDelete
  4. "Utafiti" wa kusisimua. Ingekuwa bora zaidi kama ungeweka na ushahidi ili wanaopenda kubukua zaidi wawe na rejea. Maana unapotumia neno utafiti lazima masikio ya baadhi yetu yasimame. Utafiti lazima uwe na ushahidi. Hata hivyo kazi pevu. Ni ushauri tu.

    ReplyDelete
  5. Prof. Mhango...nimekuelewa na nimeukubali ushauri wako...utafiti wangu zaidi niliufanya zamani sana kutoka kwa babu,bibi na mama yangu ambao sasa wametangulia kutuandakia mawazo..yaani ilikuwa kama simulizi vile..na leo nimeikumbuka...ni hilo tu.

    ReplyDelete
  6. Asante sana kwa utafiti huu.....nimependa kweli...inanipa hamasa siku nikienda huko nikawahoji nami nijue zaidi....maana naishi nao Tabora hata sikuwa nafahamu haya yote...asante dada

    ReplyDelete
  7. Da Eater, kwa mfano hapohapo Tabora ukiuliza zaidi utagundua kabala ya awali wilaya ya mpanda ilikuwa chini ya mkoa wa Tabora,kabla haijamegwa na kupelekwa mkoa wa Rukwa.sasa utakuta ,kuna mwingiliano wa makabila mfano,wafipa niwengi sana tabora,na makabila yaliyo kuwa katika wilaya ya mpanda.hebu fuatilia kuhusu mji wa INYONGA,uliza wazee watakwambia historia nzuri tu na utakubaliana na mimi kuhusu kabila la wanyamwezi. kaka s

    ReplyDelete