Monday, January 27, 2014

JUMATATU HII YA MWISHO KWA MWEZI HUU WA KWANZA TUIANZE NA KUMALIZA NA BAADHI MISEMO NA MAFUNZO YAKE!!!

1. Asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Hii ni kwamba hatuna budi kuwatii wazazi/walezi wetu tukitaka kuuelewa ulimwengu.
2. Si utu kwenda kwa uliyempa zawadi na kumwambia akarudishie zawadi yako.
3. Usimdharau adui ijapokuwa ni dhaifu.....Ni kwamba akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki.
4. Ili binadamu aishi na kufaulu katika maisha yake, hana busi kujitolea na kupambana na hali yoyote katika mazingira yake.
5. Kuwa na tamaa inaweza kuua. Kama wahenga walivyosema:- Njia mbili zilimshinda Fisi.
6. Mtu akifanya kazi kwa bidii hufanikiwa. Au, maskini hachoki, akichoka ujue amepata.
7. Ujinga na woga husababisha taabu na hasara kubwa ulimwenguni.
8. Wivu huangamiza familia nyingi ulimwenguni.
KAMA NAWE UNA NYINGINE KARIBU KUUNGANA NAMI...JUMATATU IWE NJEMA SANA!!!

2 comments:

  1. Da Yasinta.Misemo uliyoweka inatoa mafunzo babu kubwa, asiye na masikio na asikiye!

    Nyongeza ingine: Shukurani ya punda ni mateke. By Salumu.

    ReplyDelete
  2. Ahsante kaka Salumu...nimeipenda nyongeza yako...ni kama Tenda wema nenda zako usingoje shukrani.

    ReplyDelete