PUMZIKA KWA AMANI BIBI NAPINGI
Hapa ilikuwa 2001 nyumbani Lundusi/Peramiho. Ni baba yangu mkubwa na mke wake na mjukuu wao. Lakini kwa vile baba yangu alilelewa na wao basi sisi watoto wake tumezoea tangu utoto kuwaita babu na bibi...hii ni historia fupi sana. Kwa hiyo leo asubihi mapema nimetumiwa taarifa kuwa bibi hatunaye tena. Amekuwa ameugua muda mrefu sasa. Bibi tutakukumbuka daima kwa yote mema na mazuri uliyotuachia. Sisi tulikupenda lakini Mungu anakupenda zaidi. Lihidimiwe jina lake. PUMZIKA KWA AMANI BIBI TUPO KATIKA MAOMBI. MUNGU AIPE FAMILIA YA NGONYANI KOKOTE ILIPO NGUVU KWA KIPINDI HIKI KIGUMU.
Poleni sana kwa kumpoteza bibi yenu mpendwa,hilo ni fundisho kwetu sisi sote wanadamu kwamba, ni lazima iko siku tutaonja mauti.Mungu ampumzishe kwa Amani AMEN
ReplyDeletePole sana Yasinta na familia yote. Mungu awape faraja.
ReplyDeleteKuelekeautsjiri! Ahsante ..ni fundisho kwa kweli. Wote tupo safari moja...
ReplyDeleteUsiye na jina ....ahsanta kwa pole
poleni sana shemeji yangu...
ReplyDeletePoleni sana Yasinta kwa msiba, Mungu awatie nguvu wanafamilia wote.
ReplyDeleteRIP bibi.
Shem kajuna...ahsante.
ReplyDeleteMija...ahsante ndugu yangu. Tuzidi kumwombea bibi
Pole sana kwa kumpoteza bibi, Mungu na ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi
ReplyDeleteAhsante Edna..kwa kutupa moyo...naamini tupo pamoja katika sala
ReplyDeletePole da Yasinta! Mungu amlaze bibi mahali pema. By Salumu
ReplyDeleteAhsante kaka Salumu...na kwa taarifa mazishi ni Jumatano...
ReplyDeletePoleni sana Da Yacinta Mungu atawapa faraja
ReplyDeleteMwal. Mhango .. ahsante sana jindi mnavyotufariji ndivyo faraja inaongezeka. Mungu daina na milele...amina
ReplyDeleteDada Yasinta poleni sana, nimechelewa kukupatia pole tokana na Computer yangu kuwa na shida. Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina
ReplyDeleteAhsante kaka Nyumayo..wala hujachelewa. Chilawu vihindika
ReplyDelete