Wednesday, December 11, 2013

HUU NI MLO WANGU WA LEO MCHANA UGALI NA SUKUMAWIKI/MBOGA MABOGA!!!

Mlo aupendao Kapulya ndo huu Ugali kwa mboga maboga. Halafu sasa napenda kupika mboga hii bila mafuta wala kitunguu. Ni maji, chumvi, nyanya na pilipili kama ipo kwa mbaliiii.....mmmhhh hapo ndo utauona utamu wa mboga hii. Mboga ni kazi ya mikono yangu mwenyewe. Awekaye akiba basi hana shida kifuku kikija:-) MUWE NA JIONI NJEMA NA WALE WENYE MCHANA AU ASUBUHI BASI NA IWE NJEMA, NA USIKU UWE MWEMA PIA. Kapulya!!!!

5 comments:

  1. Duh umeanza kutupatia vyakula vyetu jamani! heri ningewahi kwako leo. Hivi hata watoto wako na baba yao wanakula hiyo mboga kama ulivyosema haina mafuta wala kitunguu? Au inakuwa yako tu wao unawaungia na mafuta? Hongera kwa mapishi.

    ReplyDelete
  2. Duh umeanza kutupatia vyakula vyetu jamani! heri ningewahi kwako leo. Hivi hata watoto wako na baba yao wanakula hiyo mboga kama ulivyosema haina mafuta wala kitunguu? Au inakuwa yako tu wao unawaungia na mafuta? Hongera kwa mapishi.

    ReplyDelete
  3. Mhh;inapendeza sana!Sukuma wiki maana yake unaweza kukata majani machache kwa kila shina mwanzo hadi mwisho wa wiki!!

    ReplyDelete
  4. Mmm napenda sana mboga hii kwa ugali lkn ckujua km pia yaweza kupokea bila mafuta ntaanza sasa, Dah umentamanisha sn!!

    ReplyDelete
  5. Usiye na jina hapo juu wote tunakula hivyo..ahsante nawe na usiwe na shaka karibu...

    Kaka Ray. .umenichekesha...

    Nancy...inapokelewa safi kabisa bila mafuta ......haya jaribu uone au karibu.

    ReplyDelete