Monday, November 25, 2013

TUANZA JUMATATU HII NA SWALI HILI KUTOKA KWA KAKA BWAYA ...KUHUSU MAISHA NA FURAHA!!!

Kama mnakumbuka mwezi uliopita niliweka picha hii hapa kibarazani na baadaye kulitokea na maoni. Na baadhi ya maoni aliyotoa msomaji mmoja ambaye ni kaka Bwaya ambaye alikuwa ameadimika kwa muda mrefu na sasa yupo nasi tena. Nachukua nafasi hii kumkaribisha Kaka Bwaya......Haya na maoni yenyewe yalisomeka hivi;-
Bwayasaid...
Tafiti zinaonyesha kuwa watu waishio katika maisha yanayoonekana kuwa duni, ndio wenye furaha zaidi. Mfano ni hawa. Swali: kwa nini? Naomba tusaidiane kujadili swali hili kwa pamoja....JUMATATU NJEMA!!!

4 comments:

  1. Habari!

    Nadhani kwa kuwa hao wanaonekana wanaishi maisha duni wana furaha kwa kuwa wao wanaishi kwa k uzingatia UHITAJI na Si UTASHI kwa maana wao wanaamini katika kupata mahitaji muhimu ya binaadamu ili aendelee kuishi mfano wanahitaji chakula si aina gani ya chakula, Mavazi si pamba za kufa mtu na nyumba za kuwawezesha kupata usingizi, ulio safi na salama na si vinginevyo. Tulio wengi tunaihsi katika maisha ya UTASHI k wa maana ya kutaka na si kuhitaji mfano badala ya kuwazia kupata chakula chenye virubishi muhimu tunaangalia pilau au chipsi kuku mayai, nk. Mavazi badala ya kusitiri mwili tunaangalia pamba za kufa mtu wenyewe mnasema nguo za bei mbaya halikadhalika.

    Kwa maneno mengine tunaishi maisha bandia badala yanaongozwa na nguvu za kimaumbile.

    Kila la kheri

    ReplyDelete
  2. Kaka Salehe kwa kweli umesema kweli wengi waishio hivyo hawachagui na mara nyingi hujishughulisha na kila wanachoona wanaweza kukifanya si kulazimisha. Nukuu "Kwa maneno mengine tunaishi maisha bandia badala yanaongozwa na nguvu za kimaumbile." mwiaho wa nukuu....nimependa msemo huu.

    ReplyDelete
  3. Nimependa sana comments za kaka Salehe, na ni kweli kabisa! Mbona umegusa wengi sana katika jamii!

    ReplyDelete