Thursday, November 21, 2013

NIMEONA TUBAKI MKOANI RUVUMA:-TATIZO LA UMEME SONGEA KITENDAWILI!!!

Katika pitapita nimekutana na habari hii ambayo imenikasirisha na kunikatisha tamaa sana maana nilikuwa katika harakati ya kuingiza umeme katika nyumba yangu. Ila najipa moyo na kuendelea ebu soma hapa habari hii iliyoandikwa Na Albano Midelo.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
 












 


 
 
 
Hapa ni baadhi ya vijana katika mji wa Songea wakifanya maandamano ya amani kudai umeme wa uhakika mjini Songea.
 
“TANESCO wanakata na kurudisha umeme bila taarifa na hata ratiba ya mgao haijulikani hali inasababisha hasara kubwa kwa wananchi ikiwemo kuungua vifaa vya umeme na vyakula vinavyohifadhiwa kwenye majokofu kuharibika’’,anasema diwani wa kata ya mjini manispaa ya Songea Joseph Fuime.
Fuime alidai kuwa tatizo la umeme Songea haliwezi kupatiwa ufumbuzi wa kudumu kwa kuendelea kutumia mashine chakavu za kufua umeme ambazo vipuri vyake vinaharibika mara kwa mara badala yake alishauri serikali kuunganisha mkoa wa Ruvuma na umeme wa giridi ya Taifa.
“Serikali iliahidi mara baada ya kuanza kuchimbwa makaa ya mawe ya Ngaka wilayani Mbinga kutajengwa kinu cha kufua umeme katika mji wa Songea hata hivyo tangu mwekezaji ameanza kuchimba makaa ya mawe hadi sasa hakuna dalili za kufungwa kinu hicho pia mwekezaji ameshindwa hata kuwalipa fidia wananchi wanaoishi katika eneo la mgodi’’,alidai Fuime ambaye pia ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Ruvuma.
Uchunguzi uliofanywa katika maeneo mengi ya mji wa Songea umebaini kuwa vibaka wakati wa usiku wameongezeka na kusababisha nyumba nyingi kukatwa nyanya za madirishani na wengine kuibiwa vitu mbalimbali zikiwemo simu za mikononi,mavazi,kompyuta za mkononi na samani mbalimbali.
Waandishi wanakwama kutuma habari zao kwa haraka na hata vituo vya matangazo vilivyopo mjini Songea vikiwemo Redio Maria,radio Jogoo,TBC Taifa, vinashindwa kurusha matangazo kwa wananchi kutokana na kukatika kwa umeme mara kwa mara.
John Mapunda mfanyabiashara soko kuu la Songea anasema Kukatika kwa umeme na kuwaka bila taarifa katika mji wa Songea kunawasababishia hasara kubwa wafanya biashara wa vyakula hasa wanaouza samaki wabichi kutoka ziwa Viktoria, Tanganyika, Nyasa na bwawa la Mtera ,wao wanatunza samaki hao katika makojofu ambayo yanatumia umeme wa TANESCO hivyo samaki wengi wanaoza.
"TANESCO katika manispaa ya Songea inaonyesha dhahiri kuwa mashine zao haziwezi kufua umeme wa kukidhi hata katika mji wa Songea,wananchi tunahoji kwanini umeme huo umesambazwa hadi mji mdogo wa Peramiho badala ya kusubiri umeme gridi ya Taifa’’,alihoji Mapunda. Frank Mbunda mkazi wa Mahenge mjini Songea anadai kuwa TANESCO wameshindwa kumaliza tatizo sugu la umeme ambalo linachangia umasikini kwa wakazi wa Songea ambao wanashindwa kufanyakazi zao za kiuchumi.
Mwanaharakati Mohamed Kudeka mkazi wa Songea anatoa wito kwa serikali kuachana na umeme wa majenereta ambao matatizo yake ya kuharibika kwa vipuri yamekuwa yanajirudiarudia na kusababisha kero kubwa kwa wakazi wa mji wa Songea ambao wanashindwa kufanya kazi za kiuchumi na kusababisha umaskini.
“Mchawi ni ugonjwa wa majenereta ambayo vipuli vyake vimechoka na kuchakaa,tumechoka na kero hii kama sio ubovu wa vipuri utasikia mafuta ya kuendeshea mitambo yamekwisha,mara fundi wa kufunga vipuri anatoka nje ya nchi TANESCO tuambieni ukweli tumechoka’,anasisitiza.
Brighton Mwandata mmiliki wa studio ya kurekodi muziki Matarawe mjini Songea anasema umeme katika mji wa Songea haujapatiwa ufumbuzi wa kudumu anashindwa kurekodi kutokana na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara wakati mwingine inamgharimu kukodisha jenereta kwa gharama kubwa. Ingia hapa kwa kusoma zaidi habari hii.

No comments:

Post a Comment