Thursday, November 28, 2013

MAISHA YA NDOA:- NIMEULIZWA SWALI HILI NA RAFIKI/MFANYAKAZI MWENZANGU!!!!

AKIWA MAWAZONI
Habari za leo Yasinta, ni siku nyingi hatujaonana. U- hali gani? Vipi familia ni wazima wa afya?  Nikamjibu, salama tu na familia wote wazima. Sijui wewe na familia yako? Akaguna...mmmhhh! Sina uhakika, sijisikii vizuri niko katika mawazo mengi. Sijisikii raha kabisa kuwa na mume wangu. Lakini ni ajabu kwa kuwa huwa hawi nyumbani muda wote. Anafanyia kazi zake mbali kidogo anaweza akawa hayupo nasi wiki moja au mbili. Kwa hiyo ilibidi nimfurahie/tufurahiane arudipo lakini ni kinyume. Yasinta, mimi bado kijana..38 na yeye 35, nipo njia panda, sifurahii maisha niliyo nayo. Pia mwenzangu naye haonyeshi kama ananijali.  Nifanye nini? Nisaidie?
Duh! Hapo Kapulya akabaki hoi maana ushauri wangu.....si wa kiataalamu wa mambo ya ndoa. Nikakumbuka Maisha na Mafanikio, kuwa nikiweka hapa kwa pamoja tutaweza kumsaidia rafiki yangu. Na ndio maana nawaombeni tujadili kwa pamoja.  Kwani kesho laweza kukupata wewe au mimi au yule n.k. Nawatakieni kila la kheri na mjadala mwema. SIKU IWE NJEMA......Kapulya

5 comments:

  1. Da Yasinta ungetupa picha kamili kwa maana ya umri wa mumewe rafiki yako, unajua uzee pia unachangia, au huko anapomaliza wiki nje utakuta ana nyumba ndogo. By Salumu.

    ReplyDelete
  2. Kaka Salum! Hapana si mzee labda sema huwa anachoka lakini kuwa na nyumba ndogo sidhani kwani anaonekana si aina hiyo. Samahani kutoandika umri na ahasante kwa kumikumbusha nimeandika sasa angalia tena labda utakuwa na maoni tofauti.

    ReplyDelete
  3. Mimi sijaelewa kidogo..yaani hatamani kuwa na mume kwa sababu gani? hapendi tendo la ndoa,Mume mkatili/hamjali/mnyanyasaji au..hapendi kuwa na mtu anayeishi naye kama MUME...
    Samahani labda Nimevurugwa na BOX..NDIYO MAANA SIJAELEWA.

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli hata mimi yananikuta hayo simpendi mume wangu akisafiri naona raha mana anakuwa mbali nami nataman hata leo hii niachane nae sina raha na haya maisha ila tu ni vile sina kazi sina pa kwenda ndio maana nashindwa naondokaje.

    ReplyDelete
  5. MAISHA YA NDOA YANAHITAJI UVUMILIVU NA BUSARA ZAIDI.WENGI WANAKURUPUKA NA KUJIKUTA WAMESHINDWA KUTIMIZA MAJUKUMU WANAYOPASWA KUTIMIZA KWA UPANDE WA MWANAMME NA WANAWAKE WENGI MAWAZO YAMEHAMIA MAFANIKIO YA HARAKA NA PESA PASIPO KUJITUMA NA KUWAJIBIKA IPASAVYO.MAISHA YA NDOA NI MAZURI KAMA UTAMSOMA MWENZIO NA YEYE PIA NA KUTIMIZIANA YOTE YALE YA MSINGI.

    ReplyDelete