Wednesday, October 23, 2013

JUMATANO YA LEO NIMEAMUA KUTEMBELEA IRINGA-ISMILA!!!

Ismila ni mojawapo wa vivutio vya utalii ambao upo ndani ya mkoa wa IRINGA yetu...karibuni wote kutembelea sehemu hii ya kumbukumbu. JUMATANO  NJEMA KWA WOTE.

7 comments:

  1. Mkoa wa Iringa uko katika Nyanda za Juu za Kusini mwa Tanzania. Mkoa huu unapakana na ukanda mkavu wa kati wa Tanzania katika upande wa kaskazini na kupakana kusini na Ziwa Nyasa. Mkoa wa Iringa umetanda kati ya latitudo 7º 05˝ na 12º 32˝ kusini, na longitude 33º 47˝ hadi 36º 32˝ mashariki mwa Meridian. Mkoa wa Iringa unapakana na Mikoa ya Dodoma na Singida upande wa kaskazini, Mkoa wa Mbeya upande wa Magharibi, Mkoa wa Morogoro upande wa Mashariki na Mkoa wa Ruvuma kwa upande wa kusini. Ziwa Nyasa linatenganisha Mkoa wa Iringa na nchi ya Malawi upande wa kusini Magharibi mwa Tanzania.

    Mkoa wa Iringa una eneo lenye ukubwa wa jumla ya km2 58,936. Wastani wa asilimia 74 ya eneo hili linafaa kwa shughuli za kilimo ambalo ni sawa na km2 43,935. Eneo linalobakia la km2 15,001 ni eneo la maji, hifadhi ya mbuga za wanyama, milima na misitu.

    ReplyDelete
  2. Kaka Ray! Ahsante kwa kuchanganua kijiografia mkoa wa Iringa.

    Nancy ....ndiyo ni pazuuri sana.

    ReplyDelete
  3. Picha nzuri sana. Sijui kuna maporomoko ya maji hapo? By Salumu.

    ReplyDelete
  4. Kwa sisi ambao hatujawahi kufika iringa, tunaomba mtuoe mwanga kuwa hiyo picha inaonyesha nini au kivutio gani? nimeshindwa kutambua. Dada Yasinta naomba sana maelezo ili nasi tufaidike kwa kujua ni nini hivyo tuonavyo.

    ReplyDelete
  5. Usiye na jina wa 5:08! Ismila ni makazi ya mababu zetu wa zamani ni makumbusho..

    ReplyDelete
  6. vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg

    ReplyDelete