Kuchuma uyoga ni kitu ambacho nakipenda sana , unakuwa na wakati mzuri wa kutafakari, pia mazoezi nahalafu unapata mboga ..Mboga hii mimi nimeipata bure leo mstuni lakini kama ningekwenda kuinunua dukani kwa kilo ni kama kwa kila shilinga 23000/= . Nami nilipata lita kama tano hivi. Sasa kazi nyingine unaporudi nyumbani ni kuusafisha na ndio hapo nafanya kutoa mchanga na takataka nyingine,,,,
Baada ya masaa matatu uyoga tayari umetolewa takataka zote na upo safi kwa kuliwa.....
...Uyoga upo kwenye plain pan tayari kwa kuandaliwa kwa ajili ya mlo wa jioni......
.....baada ya dakika tano umepungua kiasi hiki na maji mengi yamejitokeza ..naendelea kukausha maji...
---Maji yamekakamia na hapa sasa ni kuweka chumvi, sukari kiduchu kwa ajili ya ladha..na pilipili manga kidogo na kikubwa zaidi siagi kama kijiko kimoja cha mezani unakaanga kwa dakika kumi....
...baada ya hapo unaweka krimu ya maziwa na kama huna krimu basi weka unga wa ngano kijiko kimoja cha mezani na maziwa kikombe cha chai,,,,
Na mwisho mlo ukapatikana hivi:- Wali, kuku, uyoga uloungwa kama nilivyosema hapo juu ikiwa na nyanya kutoka bustanini kwetu, tango na majani ya ruccula. Na hivi ndivyo ilivyoisha IJUMAA YA KAPULYA na mpishi ni YEYE MWENYEWE KAPULYA:-) TUTAONANA TENA PANAPO MAJALIWA !!
Duuhh njaa inazidi jamanii...
ReplyDeleteUnatutamanisha sana, hivi hakuna uwezekano ukatutumia kwa posta kidogo tukaonja! By Salumu.
ReplyDeleteLadha yake ipoje cjawahi kula
ReplyDeleteAma kweli maisha na mafanikio ni kupanga na kupanga ni kuchagua.Asante kwa mlo mzuri ambao kila mdau wa kibarazani ameweza kuhudhuria japo washiriki ni wewe na familia yako.
ReplyDeletejamani jamani jamani da Yasinta jamani mbona hivyo? njaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Sasa nifanyeje na tayari chakula kimeisha! Duh! Uyoga uyoooooooga!! Leo naona umeamua kuninyima chakula chako sawa!Haya msosi mwema na familia yako tu. Mie nalia macho tu.
ReplyDeleteNachukua nafasi hii na kuwashukuruni wote mliopita hapa na kuacha yaliyo ndani ya moyo...Ahsanteni sana ila mjadala bado unaweza kuendelea...
ReplyDeleteHivi Yasinta ulipitia Forodhani? kile chuo cha hotelia?
ReplyDeleteMija HAPANA! hata iliko sijui kwanini umeuliza hivi?
ReplyDeleteJamani huwa napenda sana comments za Dada Mija, unaonyesha kuwa mcheshi sana sana! Yani uwe una comment kila wakati mana unapoteaga sana wakati mwingine. Sijui nifanyeje ili nipinge urafiki na wewe Mija.
ReplyDeletenakutamania mno, uyoga mtamu jamaniiiii duh
ReplyDeletehermes
ReplyDeleteyeezy
bape clothing
lebron james shoes
supreme outlet
curry shoes
moncler outlet
kobe basketball shoes
golden goose
yeezy
palm angels
ReplyDeletesupreme
off white outlet
bape clothing
alexander mcqueen outlet
off white
fear of god outlet
off white outlet
golden goose
golden goose outlet