Wednesday, September 11, 2013

KATIKA MAISHA NI VIZURI KUWAFARIJI MWENYE MATATIZO

Huu ni ushauri wangu mimi kwa wewe uliye na rafiki aliye na matatizo:-

1) Kama rafiki yako ana matatizo usiogope kumwuuliza hali yake kwa ujumla hata kama hali yake inaonekana si nzuri. Kama una matatizo halafu watu/marafiki wanakuuliza U HALI GANI utajisikia amani yaani kuna watu ambao wanakujali haupo peke yako.

Wakati mwingine kunatokea mambo ambayo si kweli na watu wanafikiri kuwa tayari yule mwenye matatizo amepata msaada mtu wa kuongea naye, wakati kumbe wewe upo peke yako kwa hiyo kuuliza ni muhimu sana.

2) Piga simu au nenda ili kujua mpatwa matatizo ana hali gani. Pia pika chakula, nenda kwake na mle pamoja. Wakati matatizo yanapotokea, inakuwa ngumu kuelezea vitu ulivyozoea kufanya kila siku. Kama una watoto inakuwa ngumu zaidi kuwatunza wakati upo kwenye matatizo/majonzi.

3) Onyesha upendo wako, bila kuonekana ni usumbufu kwa mpatwa matatizo, uwe nusu nusu. Usizidishe au usipunguze. HAPO NDIPO UTAWEZA. ......Huu ni mtazamo na ushauri wangu ...PAMOJA DAIMA,.

5 comments:

  1. Hiyo ni kweli mpendwa tunasema `salamu ni amani,salamu ni upendo, mkisalimiana, na kujuliana hali, mnajenga udugu, mnajenga faraja, mnaleta amani na baraka...au?

    ReplyDelete
  2. Umenena kadala wa mimi. .Asante kwa kutukumbusha.

    ReplyDelete
  3. Yesu Kristo alisoma na kusema kwamba kazi hii ya kiunabii ilimhusu: “Roho ya Bwana Mungu ni juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta, kuhubiri wanyenyekevu habari njema; amenituma niwaponyeshe wenye kuvunjika kwa moyo, . . . kuwafariji wote wanaoomboleza.” (Isaya 61:1, 2, ZSB; Luka 4:16-19) Kwa muda mrefu, Wakristo watiwa-mafuta wa leo wametambua kwamba wao pia wanapaswa kufanya kazi hiyo, nao “kondoo wengine” wanajiunga nao kwa furaha kuifanya.—Yohana 10:16.
    3 Misiba inapotokea watu huvunjika moyo na mara nyingi huuliza, “Kwa nini Mungu huruhusu misiba itokee?” Biblia hujibu swali hilo waziwazi. Hata hivyo, huenda ikachukua muda kwa mtu ambaye hajajifunza Biblia kuelewa kikamili jibu la swali hilo. Msaada unaweza kupatikana katika vichapo vya Mashahidi wa Yehova.* Lakini wengine wamefarijika kwa kusoma tu andiko fulani katika Biblia kama vile Isaya 61:1, 2, kwa kuwa linaonyesha kwamba Mungu anataka wanadamu wapate faraja.

    ReplyDelete
  4. sikuzote mwenyeshida hutafuta msaada ili asikilizwe. au hutafuta mtu wa kumsaidia shida hiyo. wasiwasi wangu unakuja pale ambapo mtu mwenye shida hyo anapo kuwa hayuko tayali shida yake itatuliwe ama asaidiwe.hayuko tayari kivipi,? mwenyeshida maranyingi hupenda kuonewa huruma hivyo huwa tayari katika akili yake anamsimamo fulani juu ya shida ile,kwa sisi binaadamu, kwa hulka yetu/zetu maranyingi hujisikia kuwa na huruma na mtu huyo tukidhani ndiyo tuna msaidia kumbe inakuwanifaraja au msaada wa muda. muhimu siyo kumuonea huruma bali ni kumuwezesha mtu hyo mwenyeshida ajijuwe kwanini amefika hapo kutokana na shida hiyo au tatizo hilo. mpokee mtu huyo mwenyeshida jaribu kuvaa "viatu"vyake ili ujuwe nini tatizo au nini shida yake bila hivyo huruma haita saidia kumjenga mwenye shida au tatizo.kaka s.

    ReplyDelete
  5. Ni kweli kabisa dada Yasinta.

    ReplyDelete