Kama wengi mnakumbuka mwezi Novemba tarehe 3 mwaka jana nilifiwa na mama mkwe wangu ghafla tu kwa kujikumbusha inga
hapa. nachotaka kusema hapa ni kwamba ijumaa ya tarehe 16/8 -13 ndiyo tumemzika mama Irene. Sababu kubwa ya kusubiri muda mrefu kiasi hiki ni kwamba:- Kwanza ardhi ilikuwa ni ngumu kuchimba kaburi baridi kali mno..Pili ni kwamba mwili wa mama Irene ulichomwa moto. Hakika hii ilikuwa mara yangu ya kwanza kuona utamaduni huu. Kwa hiyo kwenye hicho chombo hapo chini ni masalio ya mwili wa mama Irene
Mwili/majivu ya mama Irene
Hapa pia na mishumaa imewashwa
Na hap ndiyo safari yake ya mwisho kwenye nyumba ya milele. Walichimba kashimo tu ili kutosheleza hicho chombo kilichokuwa na majivu. Na ni kaburi alilozikwa baba mkwe pia kwa hiyo wote wamezikwa katika kaburi moja..Duh ama kweli tembea uone mengi ila kuchomwa moto..mmmhhh sijui!! UPUMZIKE KWA AMANI MAMA YETU MPENDWA IRENE.
Da Yasinta! Mi najua kuchomana moto ni kwa mabaniani tuu, kumbe kuna wazungu wanachomana wakifa. By Salumu.
ReplyDeleteMmmhhh Poleni sana..
ReplyDeleteMungu awazidhie amani na faraja tele. Pole sana.
ReplyDeleteYasinta hakika umetembea na sasa umeyaona na umekumbuka maneno ya mama yako Alana.Binti yangu kuwa uyaone na sasa usisahau kuwa umependa boga na kifutacho ni..........................................!
ReplyDeletePOLENI SANA!
Duh, kweli hiyo ya kuchoma moto mila yake ni kali, poleni sana kwa kupotelewa na mama mkwe, Mungu azidi kuwafariji
ReplyDeletePole sana ila kwenye kuchomwa moto mmhh kwa hiyo na ww ukifa watakuchoma moto!
ReplyDeleteKaka Salumu:- Hapana hii mila ipo sana huku tena afadhali ya sisi tumezika majivu wengine huwa wanayapeperusha ziwani, mstuni au mlimani.
ReplyDeleteSande/udalike! Kachiki!
Usiye na jina! Ahsante sana.
Ahsante kaka Ray!
Ester! Nakwambia nikali haswa niliwahi siku moja kushuhudia wakichoma mtu nusu nizimie..Halafu wanamchoma na sanduku ambalo labda limeghalimu pesa nyingi. Na halafu kwangu haileti maana au huwa najiuliza sasa haya majivu si yamechanganyika na mbao? ila basi tu....
Shalom! Ahsante, ni kweli kuchomwa moto mmmmhh ...Hapana sitachomwa moto ...
wanathamini ardhi ona hapa bongo makaburi kibao yamebana nafasi
ReplyDeletewanathamini ardhi ona hapa bongo makaburi kibao yamebana nafasi
ReplyDeleteUsiye na jina wa 21/8/2013 at 5:58 PM usemapo wanathamini ardhi una maanisha nini?
ReplyDeleteDada Yasinta, cremation nadhani ipo siku itafika tuu Tanzania. Gharama zake ni nafuu ukilinganisha na utaratibu wa kuzika mwili mzima. Ni utamaduni mpya, na wengi wetu tunaushangaa , lakini kidogo kidogo utazoeleka na kukubalika kwenye jamii.
ReplyDelete