Nadhani mnakumbuka wiki iliyopita nilikuwa kwenye kasafari kidogo kutafiti historia ya nchi kwa mfano kame hii na sikuishia hapa niliendelea na nikapata kuona haya pia ......
Hapa ni makumbusho ya redio ..si wote tunakumbuka zamani redio ilikuwa ni kitu muhimu sana kulikuwa hakuna njia nyingine kupata habari zaidi ya redio labda na magazeti...Hapa uliweza kutuma telegram na kudhalika ..
Na halafu nikashuhudia jinsi mdada huyu alivyoweza kutumia mikono yake kwa kazi hii ya kutengeneza gilasi kwa njia ya kupuliza. Hakika Mungu amempa kila kiumbe uwezo/kipaji chake. sikuishia hapa ...
...nikaendelea na halafu nikapata kuona hifadhi ya ndege. Kwa muda wa wiki moja nimepata kuona mambo yote haya na nimeona si vibaya kama nikiwajuza na wenzangu. Maana elimu kugawana. Jumatatu njema kwa wote.
Asante kwa fadhili zenye upendo na rehema da'Yasii.Kutoka katika papachi za moyo umeamua kuweka mbele yetu kile ambacho umekiona katika msafara wako.Asante sana!!
ReplyDeleteTunashukuru sana jamani nasi kuyajua hayo japo kwa picha, ubarikiwe Da yasinta. Tupo pamoja.
ReplyDeleteKweli tembea uone. Hongera sana Yasinta kwa kututembeza na sisi tulio mbali...
ReplyDelete