Tuesday, July 23, 2013
SWALI LILILONISUMBUA SIKU YA LEO...!!!!
Nimeamka asubuhi hii na nimemshukuru Mungu kwa kunilinda. Nikaona ngoja ninyooshe viungo:- Yaani nikaende nje kama kawaida yangu kukimbia, nimekimbia, nimekimbia mara nikakutana na mkimbaji mwingine naye kawaza kama mimi anakimbia. Sasa hapa kitu kilichonipa swali ni kwamba mdada huyu alikuwa akikimbia na mbwa wake ambaye amemfunga kamba shingoni. Swali likanijia huyu dada ana uhakika kama huyu mbwa/kambwa anataka kukimbia? Maana niliona kama mbwa mwenyewe hata hakufurahia. Nikataka kusimama na kumuuliza.....lakini nikaacha. Muda wote nilipokuwa nakimbia swali lilizidi kunisumbua hivi kweli yule mbwa alipenda kukimbia? Na pia nikazidi kuwaza....Nikaona niwape na wenzangu haka kakisa....TUSITENGANE TUWA TUNAKUMBUKANA. PAMOJA DAIMA SIKU NJEMA. KAPULYA!!
Sulemani aliendelea kuandika hivi katika kitabu cha Mhubiri: “Nilirudi, nikaona chini ya jua kwamba si wenye mbio wanaoshinda katika mbio, wala wenye nguvu wanaoshinda katika pigano, wala pia wenye hekima wanaopata chakula, wala pia wenye uelewaji wanaokuwa na utajiri, wala wenye ujuzi wanaopata kibali.” Kwa nini? Alieleza hivi: “Kwa sababu wakati na tukio lisilotazamiwa huwapata wote.”—Mhubiri 9:11.
ReplyDeleteHongera kwa mazoezi. .mbwa hata kama hajapenda mwenye mbwa kapenda basi analazimishwa tuu.. Hii inatufundisha hata sisi. . Upendacho wewe si lazima wengine wapende au fuate. . Basi si vyema kulazimisha watu/watoto wafuate kila maamuzi/matakwa, mapenzi yako.
ReplyDeleteYasinta nawe kwa kuwaza!!!
ReplyDeleteHukumchukua kideo ili tuone halafu ndo tutathmini?
Binafsi bado sipati picha mbwa akikimbia bila kupenda anafanyaje, ila nadhani mnyama si lahisi kumlazimisha kitu akikataa huwa amekataa na ukimlazimisha tehgemea lolote.
Mshkaji kumbe umeanza kukimbia? nami ngoja nijipange nianze next week.
Jioni njema.
Kaka Ray...ahsante kwa neno.
ReplyDeleteKachiki...ulichosema ni cha kweli lakini pia unajua kuna watu wanaopenda kulazimiasha kwa vile wao wanapendsa basi wanataka na wewe mwingine upende si uungwana kwa kweli.
Mija! Si unajua mie ni kapulya na halafu mtu unawaza kila wakati...
Sikuchukua video aise kwa vile ilikuwa ghafla alinitokea mbele yangu ..Sijaanza ninakimbia kila nipatapo muda ..Karibu kiwanjani tufanye mashindano...LOL. Jioni njema nawe pia dada mkuu msaidizi:-)
Tumepata somo kuwa sio kwamba kila ukipendacho WW na mwenzako anakipenda na sio kwa wanyama Tu hata binadamu tuwe makini kwa hilo ndugu zng, Da yasinta tumefurahia somo MN jibu lako ni funzo kwetu.
ReplyDeleteTumepata somo kuwa sio kwamba kila ukipendacho WW na mwenzako anakipenda na sio kwa wanyama Tu hata binadamu tuwe makini kwa hilo ndugu zng, Da yasinta tumefurahia somo MN jibu lako ni funzo kwetu.
ReplyDeleteAsante na kwako pia cku njema.
ReplyDeleteMi nafikiri alikuwa hajamlazimisha huyo mbwa kukimbia, ila mbwa mwenyewe alitaka iwe hivyo kwani imezoeleka kwa baadhi ya mbwa kumfuata mwenye mbwa pindi anapotaka kuondoka na kumwacha.
Mi kwa mtazamo wangu hakumlazimisha mbwa kukimbia, bali ni kieleele cha mbwa mwenyewe.
Nancy na Phocus ahsanten sana !
ReplyDelete