Wednesday, July 10, 2013

PICHA ZA WIKI:- KAPULYA NA NYWELE ZAKE!!

Hapa ni ijumaa wakati nasaka msusi...na ghafla jumamosi akanipa taarifa atanisuka kwa hiyo kazi sasa ni kufumua hizo nywele za kimasai...kazi ikaanza jumamosi..
 ..na jumatatu mzigo umekwisha sasa kazi kuchana eeeh bwana wewe si unaona hapa na afro yangu..leo jumatano ndo naenda kusuka ...nikirudi nitawaonyesha vipi imekuwa...Haya basi baadae:-)

11 comments:

  1. Dah umetokelezea sana na hiyo afro pia nimekependa rangi yako chocolate dada.

    ReplyDelete
  2. Yaani Dada yangu from another mother unapendeza kote kote,uwe umesuka au afro...nasubiri kwa hamu kuona msusi alivyokupendezesha.

    ReplyDelete
  3. Umependeza Kadala. . Tusubiri picha mpya.

    Kadala unajua kusuka?

    ReplyDelete
  4. achilia hilo afro kwa mwezi mzima tujinome maana na hapo unapendezeya!

    ReplyDelete
  5. Ni kweli Wambura nakuunga mkono kuwa dada Yasinta ungechana hata kwa muwa wa mwezi mana unapendeza pia na afro, unasuka mabutu usiku na asbhi ukiwa unatoka au kazini au muda wa kutoka wowte unafumua na kuchana afro inabakia safi tu na hivi sasa ni summer hali ya hewa nzuri hata kwa nywele sio kama winter mana huwa zinakatika mno. Pia una bahati ukisuka na ukifumua nywele zako hazikatiki. Tunasubiria style mpya ya nywele kwa hamu sana.

    ReplyDelete
  6. Dada wakati mwingine ni vizuri kupumzika na rasta na kuchana au pia kufanya style nyingine hii inakusaidia kurelaxisha muscules za kichwani mana naona wewe mwaka mzima ni rasta, je umewahi kulifikiria hilo? Jaribu hata kupumzisha misuli ya kichwani. Haya ni mawazo yangu tu.

    ReplyDelete
  7. Mhhhhhhhhh;hakika mambo yote ni mema na sifa zipae hadi mbinguni wa Muumba wa mbingu na ardhi.Hongera kwa matiti uliyonyonya na mikono salama iliyokukuza.

    ReplyDelete
  8. Yasinta hizi rasta ulitoka nazo bongo nini?

    Hivi umeshawahi kufikiria kusuka rihanna style..(nakuchokoza dada)nasubiri jibu..

    https://encrypted-tbn1.gstatic.com/images?q=tbn:ANd9GcT6JqNzvzLeE5R2QDaSZu5UIbwk_r6kkt8W3GoTiYVkxwJYB_IW

    ReplyDelete
  9. Ahsanteni wote jamani...kama muonayo hapo juu nismeshasuka....
    Mija dada mkuu msaidizi. ..kweli ae mchokozi. .Rihanna ndo nini? Ndiyo nilisika bongo.

    ReplyDelete
  10. Nimekuwekea hiyo link uone Rihanna..

    ReplyDelete