Wednesday, July 10, 2013

BAADA YA MASAA MATANO NA HUU NDIO MWANEKANO MPYA WA KAPULYA!!!

 Hapa ni kichwa kizima, picha imepigwa kwa juu kuonyesha mwonekano wote...masaa matano nimekaa bila kuinuka na matokeo ndio haya..
Na hapa ni kwa mbele...mnaona kapulya alivyochoka si mchezo lakini nimefurahi nimeweza kusukwa maana zile nilisuka mwezi februari:-)..Dada Natalie kutoka Kongo  ni mwepesi ajabu...Sijui hizi nitakaa nazo muda gani:-)
 
 
Haya nawatakieni jioni njema ..Panapo majaliwa tutaonana tena...Kapulya ndani ya poziiii:-)

20 comments:

  1. Umependezaje mdada..

    Ngoja nami nikasuke zangu..

    Eti kama hizo ni bei gani?

    ReplyDelete
  2. Kwa mapozi na mapozi;mhhhhhhhhh!!

    ReplyDelete
  3. Mija! ahasante. ...haya kasuke twasubiri. Bei yake inavumilika nitakuandikia :-(

    Kaka ray! :-D

    ReplyDelete
  4. Hongera! Umependeza ila sikuwa najua kuwa kusuka kwaweza kuchukua muda mrefu namna hiyo? Saa 5!Yaani mtu anaruka na ndege toka Dubai hadi Dar anafika na kupika wewe bado unasukwa tu.Kumbe kupendeza kuna gharama Kadala,bee,Mwee!

    ReplyDelete
  5. Kachiki sande alo. Ila bodi inauma usiombe.

    Usiye na jina! Ahsante sana...hivi leo hup si muda mrefu kwa kawaida inachukua siku nzima ila huyu dada mkono wake mwepesi. Halafu za kimasai ndo zonachukua siku hadi mbili. Ukitaka kupendeza yabidi Uvumilivu. :-D

    ReplyDelete
  6. nilistuka ile heading ya habari ya saa tano mfululizo bila kuinuka. nikaogopa! kumbe ulikuwa unasuka rasta, ha haaa haaaa! unyambili sana "Rasta woman" big up

    ReplyDelete
  7. Hej yasinta....hade vägarna förbi och så fina bilder du ha uppladdat av dig själv.

    ReplyDelete
  8. Naomba kukuuliza je ukimaliza kusuka haziumi? au kusikia kama kichwa kinauma? au kuvuta? na chini anasokota akinza kusuka au anasuka kama butu tangu chini? nataka kujua tu, kingine je hizo rasta ni za Tz. kama alivyouliza da Mija mana naona kama hazina tofauti na ulizofumua? Ni hayo nikipata majibu ntashukuru sana.

    ReplyDelete
  9. Mbona unapenda sana rasta maana naona kila ukienda kusuka unasuka hizohizo jaribu kubadilisha staili ya nywele cio mpaka ukiwa kwa mbali wanajua yasnta yule ulizo fumua na hizo hazijatofautia au ushajua zinakupendeza basi ni bandika bandua samaha ni maoni tu dada

    ReplyDelete
  10. Nancy ahsante ndugu yanguu

    Kaka Nyumayo pole kwa hilo. Usengwili kupita hapa na kujova ga mumtima.

    Tack V:-D

    Usiye na jina wa 6.41AM zinauma ila ndo hivyo tena. Inategemea wamasai wanaanza kusokota ba huyu dada aöianza moja kwa moja kama butu tangu chini. Na ndiyo nilinunua bunda kadhaa na zina tofauti zile nilizofunua ni sangita kwa mtindo/msuko wa kimasai na hizi ni za kawaida.
    Kaka Chacha:-D

    Usiye na jina wa11.27 AM. Zina utofauti kama nilivyosema hapo juu.

    ReplyDelete
  11. Hongera na pole kwa kukaa masaa yote hayo, ...niwaulize, ukishasuka hivyo ina maana huoshi hizo nywele tena, hakuna kuwashwa maana unakaa nazo siku nyingi bila kuipitisha maji au sio?

    ReplyDelete
  12. Emu-tvree !ahsante...kuosha ni kama kawaida
    .kwanini nisionshe?...nakaa nazo muda mrefu kwa vile sina msusi nk

    ReplyDelete
  13. Swali la M-3 linaonyesha kabisa bado hajaoa...Kweli si kweli kaka M3?

    ReplyDelete
  14. Umependeza Dada yangu,Nakutakia weekend njema wewe pamoja na familia yako

    ReplyDelete
  15. Mija! Yawezekana tusubiri jibu...lol
    Manka! ! Ahsante wiki end yangu ilikuwa njema.
    Dada M! Ahsant sanaaa. Na karibu tena.

    ReplyDelete