Wednesday, July 24, 2013

MAPISHI:- LEO MLO NILIOANDAA NI HUU ANGALIA HAPA CHINI !!!!

 Hapa ni mishikaki ya kidali cha kuku ambayo imeandaliwa kwa kuwekwa kwenye mafuta kidogo,soya kidogo, kitunguu saumu,tangawizi na limau. Na baada ya hapo ikatundikwa kama mishkaki kama muonavyo tayari kwa mchomo....
 Na hapa ni sahani zitakazotumika kwa vile tutakuwa nje basi vilibebwa vingine pia kwenye sinia hilo. ambavyo ni nyanya, tikiti maji, njegere mbichi kutoka bustanini na zeituni za rangi mbili kijani na nyeusi.
 Mishkaki imeweka kwenye moto tayari kwa kuchomwa na dada Kapulya ...bahati mbaya haonekani kwenye picha kwani anakimbia ndani na nje kuangalia wali....
 Baada ya dakika kumi mishkaki inaonekana hivi nimechoma dakika tano kila upande..tayari kuliwa ..KARIBUNI TUJUMUIKE....
Na hii ni sahani ya Kapulya mshkaki mmoja, tikiti maji na nyanya pembeni, njegere, wali, na kitamu zaidi MCHICHI KUTOKA BUSTANI YANGU....MMMMMHHH. Hakika kulima raha..si mnaona eeeeh ..KARIBUNI ..ILA NIMEUKOSA UGALI..NITAANDAA KESHO NA MBOGA MABOGA:-)..HAYA MUWA NA JIONI/USIKU AU LABDA MCHANA AU ASUBUHI NJEMA. KAPULYA/KADALA.

13 comments:

  1. KADALA..Kumbe nawe mzuri kwenye mapishi...Hongera sana na mnibakishie..naja huko!!!!!

    ReplyDelete
  2. Eeeeeh weewe kachiki hukujua hili mpaja kuchoma nimo...wahi twakudsubiri ..

    ReplyDelete
  3. Kweli KADALA Unafaa haswa..naja..

    ReplyDelete
  4. Hongera kwa mapishi ambayo wengine tumekula kwa macho! Ila kama kawaida yangu usisahau kunibakishia.

    ReplyDelete
  5. Msosi nangae, msondo na biso!Hakuna raha kama kujipikia mwenyewe. Hongera da Yasinta.Wabheja sana. By Salumu.

    ReplyDelete
  6. Da yasnta wenzio swaumu watutamanisha

    ReplyDelete
  7. Huu hakika ni mlo ndani ya mlo!!

    ReplyDelete
  8. Yasinta usisahau kunipostia chakula hicho jamani! vyombo ntavituma kukurudishia.

    ReplyDelete
  9. Da yasinta mate yamenijaaje mdomoni upo juu kwenye mapishi hongera sana

    ReplyDelete
  10. Duh, unanitamanisha wakati tumefunga...lol

    ReplyDelete
  11. Ni furaha ilioje kuwa nanyi
    Pro masangu karibu sana sana tena nilikutangaza umepotea nashukuru umerufi. Si unajua ndugu......mija ......kawaida tu.

    ReplyDelete