Thursday, July 18, 2013

KILIMO CHA BUSTANI NA MAUA CHA DADA YASINTA...KARIBUNI !!!!!

Habari zenu..kuna wengi wameniuuliza vipi kuhusu bustani pia mapishi nipi na bustani ipi ila pilikapilika ni nyingi na hizi likizo lakini leo nimeona sio mbaya nichukue muda na kuwaonyesha maendeleo ya bustani yangu...Karibuni
 
 
 Nyanya zimeanza kukomaa karibu nitakula
 Kushoto ni mchicha na kulia ni figiri  mnaona ilivyokua
 Njegere zimeanza kuchanua
 Viazi mviringo(matosani)  navyo vimwanza kuchanua
 Mdada huyu ni mpenzi wa maua pia mawe hapa mnaona maua yako yanavyoendelea.
Kwa kuwa mtundu nikajaribu kupandikiza pilipili pia maana pitiku bila pilipili mmmmhh na matokeo ni haya
Sikuchoka nikajaribu kupandikiza dodoki  Nanasi na tangawizi---Dodoki kwenye hicho chombo cha bluu, nanasi chombo cha blauni na tangawizi chombo cheupe. Kwa msingi kwa kweli unaweza kupanda kila kitu na kuvuna. Haya nawatakieni Alhamisi njema na karibuni kula mazao.
 

10 comments:

  1. Jamani yaani nakutamania Sana dah hongera Sana, bustani inapendeza hadi raha yaani ngoja nami nijaribu

    ReplyDelete
  2. Jamani yaani nakutamania Sana dah hongera Sana, bustani inapendeza hadi raha yaani ngoja nami nijaribu

    ReplyDelete
  3. Jamani KADALA Nimetamani saana.. Mmmhh mnajinoma.. Kazi nzuri sana dada wa mimi Hongera sana.

    ReplyDelete
  4. Hóngera kwa kilimo kwanza. Yaani mbona mie natamani sana nikiona mboga mboga hizo. Kweli wewe ni mtundu na nanasi kwenye container, ila likiwa tayari utupigie picha kabla hujalimenya na tualike tuje kufaidi pamoja na mbona na vyote. Nakutakia siku njema.

    ReplyDelete
  5. Hongera da Yasinta kwa bustani maridadi na iliyobaki ni kupanda mipapai. Ramadhani njema! By Salumu.

    ReplyDelete
  6. Ndigu zangu wote mnakaribishwa kujumuika nasi katoka kula hizi mboga ila nyanya bsdo kidichu.....halafu nimecheka kweli kaka Salumu kupanda mapapai mmmmh hata nitajaribu. Ramadhani njema nawe pia.

    ReplyDelete
  7. Jitihada zako wewe mwanamke wa Kingoni zinathaminiwa sana na sisi wadau wako.Kamwe usilegeze mkono wako kwa jembe halimtupi mkulima.Hongera sana Kapulya Kadala na endelea na masimulizi yenye msingi wa biblia hapa chini wakati huu wa wikiendi njema pamoja na familia yako iliyohanikizwa na fadhili zenye upendo na rehema.
    ====================================
    1. Je, bustani ya Edeni ilikuwa mahali halisi?

    Kwa nini watu wana shaka kuhusu jambo hilo? Huenda falsafa ilichangia kuwapo kwa shaka hizo. Kwa karne nyingi, wanatheolojia walikuwa wakifikiria kuwa bustani ya Mungu bado ilikuwa mahali fulani. Hata hivyo, kanisa liliathiriwa na wanafalsafa Wagiriki kama Plato na Aristotle, walioamini kuwa hakuna kitu kikamilifu duniani. Ukamilifu ungeweza kupatikana mbinguni pekee. Kwa hiyo, wanatheolojia wakakata kauli kuwa lazima Paradiso ya kwanza iwe ilikuwa karibu na mbinguni.* Wengine walisema kuwa bustani hiyo ilikuwa juu ya mlima mrefu sana hivi kwamba haingeweza kuathiriwa na dunia iliyopotoka; wengine walisema ilikuwa katika Ncha ya Kaskazini au Ncha ya Kusini; nao wengine walisema ilikuwa karibu na au juu ya mwezi. Haishangazi kuwa simulizi kuhusu bustani ya Edeni lilianza kuonekana kama jambo la kuwaziwa tu. Wasomi fulani wa kisasa wanasema kuwa habari kuhusu mahali ambapo Edeni ilikuwa ni upuuzi mtupu, wakisisitiza kuwa hakujawahi kuwapo na mahali kama hapo.

    Hata hivyo, Biblia haielezi kuhusu bustani ya Edeni kwa njia hiyo. Katika Mwanzo 2:8-14, tunajifunza mambo kadhaa kuhusu eneo hilo. Bustani hiyo ilikuwa mashariki ya eneo linaloitwa Edeni. Maji katika bustani hiyo yalitoka katika mto ambao ulikuwa chanzo cha mito minne. Majina ya mito hiyo yote minne yanatajwa na pia maelezo mafupi kuhusu mahali ilikoelekea. Wasomi wengi wametamani sana kujua habari kuhusu eneo la Edeni, hivyo wengi wao wametumia sehemu hii ya Biblia kujaribu kutafuta eneo hilo la kale liko mahali gani. Hata hivyo, wasomi hao wametoa maoni mengi tofauti-tofauti kuhusu eneo hilo. Je, hilo linamaanisha kuwa maelezo halisi kuhusu eneo la Edeni, bustani hiyo, na mito yake ni uwongo au ni hadithi tu?

    Wazia: Matukio ya simulizi la bustani ya Edeni yaliyotokea miaka 6,000 hivi iliyopita. Musa ndiye aliyeandika simulizi hilo, na huenda alitumia masimulizi yaliyopitishwa kwa mdomo au hata maandishi fulani yaliyokuwapo wakati huo. Hata hivyo, Musa aliandika simulizi hilo miaka 2,500 hivi baada ya matukio hayo. Tayari matukio katika Edeni yalikuwa historia ya kale. Je, baada ya karne nyingi kupita, huenda alama hizo kuu kama mito imebadili mikondo yake? Uso wa dunia unabadilika kila mara. Eneo ambapo bustani ya Edeni ilikuwa linaathiriwa sana na matetemeko ya ardhi—asilimia 17 ya matetemeko yote duniani, yanatukia katika eneo hilo. Katika maeneo kama hayo, mabadiliko katika uso wa dunia ni jambo la kawaida. Zaidi ya hayo, huenda Gharika ya siku za Noa ilibadili uso wa eneo hilo katika njia ambazo hatuwezi kuzielewa leo.*

    Hata hivyo, kuna mambo machache ya hakika tunayojua: Simulizi la kitabu cha Mwanzo linataja kuwa bustani ya Edeni ilikuwa mahali halisi. Mito miwili kati ya mito minne inayotajwa katika simulizi hilo—Efrati na Tigri, au Hidekeli—bado ipo hadi leo, na baadhi ya vyanzo vyake viko karibu-karibu. Simulizi hilo linataja majina ya maeneo ambapo mito hiyo ilipitia na hata inataja kihususa maliasili zinazojulikana sana katika eneo hilo. Habari hizo ziliwasaidia Waisraeli wa kale waliosoma simulizi hilo kuelewa mambo mengi.

    ReplyDelete
  8. Ahsante kaka ray kwa ufafanuzi kuhusu bustani.

    ReplyDelete
  9. Inaonekana udongo wako unarutuba sana angalia mpilipili ulivyona majani mapana halafu rangi imekolea

    ReplyDelete
  10. Kaka Bennet! ina rutuba kiasi chake natumia samadi , hasa ya ngómbe na kuku....Ahsante

    ReplyDelete