Thursday, June 20, 2013

MDADA KAONA KUWA MODE KWA SIKU MOJA SI MBAYA..AU SIJUI NIBADILI KAZI:-)

 Hapa sijui ndo madoido/madolido au sijui alikuwa anapigana kareti mweee kaaazi kweli
 Na hapa bonge la poozi na miondoka mwanana..hapa ni Jangwani seabreeze resort Dar es salaam. Ni sehemu nzuri sana kupunga upepo..ilikuwa mwaka huu mwezi wa mbili.
 Mmmmh...hizi nywele za kimasai zinawasha ..maana ndo nilikuwa nimesuka tu hapa:-)
Na hapa sijui anasoma misa maana utafikiri anasema bwana awe nanyiii...ni Jangwani tena ...Jioni njema. Na kwa taarifa fupi ni kwamba mkiona nipo kimya msiwe na shaka nipo lakini nitakuwa likizo na ndiyo muda wa kupumzika na kuwa na familia..TUSITUPANE NDUGU ZANGU.. TUTAONANA TENA PANAPO MAJALIWA...Kapulya

14 comments:

  1. Hongera model Yasinta, ila hiyo picha ya kwanza mie sijaelewa umesimama au? Mbona miguu hivyo? Na hiyo ya juu ni gauni umekuja au blauzi? Mana siielewi elewi! Nifahamishe Yasinta. Ila duh u model sijui kama utauweza mana na kofia tena kichwani, duh.

    ReplyDelete
  2. Hongera model Yasinta, ila hiyo picha ya kwanza mie sijaelewa umesimama au? Mbona miguu hivyo? Na hiyo ya juu ni gauni umekuja au blauzi? Mana siielewi elewi! Nifahamishe Yasinta. Ila duh u model sijui kama utauweza mana na kofia tena kichwani, duh.

    ReplyDelete
  3. Yaaani KADALA Leo umeamua saana..yaani kila kitu chako leo..nachekatuu nikiangalia simu smna mbavu..huku kumependeza pia...ok nitarudi....

    ReplyDelete
  4. Usiye na jina hapo juu kwanza ahsante. Pili hiyo picha ya kwanza nimesimama na hiyo soio gauni ni sweta na ni mbwembwe tu
    Kwa nini sitaweza hiyo kazi? Kwami hujawahi kuona model wana kofia?

    Kachiki! Usicheke sana..
    Vipi nomechemsha au?

    ReplyDelete
  5. hapana hujachemsha kabisaa..napenda na kufurahi vituko vyako@

    ReplyDelete
  6. hapo umtokelezea model wa ukweli! nikija wiki ijayo ntakupa interview ya kujiunga na model wa Swahili Abroad! Bila shaka utashinda! haaaa!haaa!haaaa!

    ReplyDelete
  7. Ongeza picha zaidi Yasinta...

    Ila picha ya kwanza imekaa ki-kareti zaidi..

    Kumbe fani unaziweza Model Yasinta, hongera sana mwanakwetu.

    ReplyDelete
  8. Dada Mija umeongea name nakuunga mkono kweli hiyo picha ya kwanza nadhani wakina Camilla na Erick walisogea mbali kama sio kukimbia mana hapo ni ku-koswakoswa na mama! Nadhani uliset camera ikupige mana nani angekusogelea hivyo sio rahisi eh! Haya pia tunaomba picha zaidi. Nakutakia mapumziko mazuri wakati huu wa summer.

    ReplyDelete
  9. Picha zote umependeza sana Dada Yasinta.Nakutakia mapumziko mema wewe pamoja na family yako.Enjoy....

    ReplyDelete
  10. Kachiki, kaka justin, dada mkuu msaidizi, usiye na jina na Manka ahsante na samahani kuchelewa kujibu sehemu niliyokuwepo haikuqezekana..pamoja daima.

    ReplyDelete
  11. Binadamu mmoja na vipaji lukuki??

    ReplyDelete
  12. kaka Ray? unaweza kugfafanua hapa? natanguliza AHSANTE ZANGU:-)

    ReplyDelete
  13. Binadamu mmoja:Yasinta
    Yasinta huyu ambaye ni binti/mama wa Kitanzania mwenye asili ya Kingoni ni binadamu mwenye ubunifu/vipaji visivyo na idadi(lukuki) kamili.
    Hongera sana wewe Yasinta binti Dadi Ngonyani.

    ReplyDelete
  14. Oh! Kumbe. ..kaka Ray ahsante kqa ufafanuzi ubarikiwe.

    ReplyDelete