Friday, May 24, 2013

MHASHAMU ASKOFU MKUU WA JIMBO KUU LA SONGEA DKT NORBERT WENDELIN MTEGA ASEMA AHSANTE JIMBO KUU LA SONGEA

Na, Stephano Mango, Songea
JUMATANO Mei 15, mwaka 2013 ni siku ya historia kubwa na ilioyo dhahiri kwa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Songea na kwa Waamini wote wa Yesu Kristo na wote wenye mapenzi mema
Ni siku pekee ambayo haikutarajiwa na Wateule, Watakatifu na Wanakanisa pale Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea Dkt Norbert Wendelin Mtega alipoamua kuwatangazia Taifa la Mungu kustaafu ( Kujiudhuru) nafasi yake hiyo
Aliamua kuwatangazia uamuzi wake huo Viongozi mbalimbali wa Kanisa Majira ya saa saba Mchana Hanga Monasteri iliyopo Wilaya ya Namtumbo Mkoa wa Ruvuma nje kidogo ya Wilaya ya Songea, siku ya Jumatano Mei 15, 2013
“…kwa kuzingatia hali yangu ya afya , kwa kuzingatia jinsi nilivyoonja utendaji wangu unavyoonyesha dalili za kuchoka na pengine kuzorota nikiwa katika mwaka wangu wa 28 wa Uaskofu kwa hiari yangu kabisa niliamua kumuandikia barua Baba Mtakatifu ili aniruhusu kustaafu kabla ya kufikia umri wa sheria na kanuni za kustaafu rasmi” alisema Mtega
Alisema kuwa nafurahi kwa kuwa Baba Mtakatifu leo amenijibu na kunikubalia ombi langu na dakika hii mbele yenu natua jukumu lote la Uongozi juu ya Jimbo Kuu la Songea
Kwa hiari yangu na kwa kuashiriwa na hali ya afya yangu na jinsi kazi inavyonielemea kupita uwezo wangu wa awali, nafanya hivyo kwa ajili ya ustawi wa Taifa la Mungu, na hasa Kanisa lililoko Songea kwa hiyo mimi staki niwe kikwazo na hoja ya Jimbo kuzorota katika siku za mbele
Alisema kuwa kuanzia sasa Msimamizi wa kitume wa Jimbo kuu la Songea katika kipindi ambacho ambaye ameteuliwa na Baba Mtakatifu ni Mhashamu Baba Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa
Ni msimamizi kwa kuwa ataliongoza Jimbo kuu la Songea katika kipindi ambacho Baba Mtakatifu anapitia mchakato wake wa kumteua na kumtuma rasmi Askofu Mkuu mwingine wa Songea. Endelea kusoma zaidi hapa

No comments:

Post a Comment