Hapa ni baadhi ya matu ya bustani yangu ...maandalizi yameanza..leo mnaona udongo tu hapa baada ya wiki mtaona mimea....
Katika maisha inabidi uwe mtundu hapa nilikwisha andaa baadhi ya miche kama vile NYANYA na Miche ya mboga ZA MABOGA,,ujanja eeeehhh
Mdada/kapulya hapendi shughuli za bustani za mboga tu ni mpenzi sana wa bustani sana wa bustani za maua kama mnavyoona hapa na mawe pia....kwa hiyo msione nipo kimya nipo ...daima pamoja...anayejisikia kuja kusaidia anakaribishwa..majembe yapo mengi tu:-)
KWELI PAMEVUTIA DADA, HADI RAHA.....TUTAJUMUIKA KWA MACHO, KAZI NZURI SANA YA MIKONO
ReplyDeleteEster! na karibuni patavutia zaidi..Nashukuru kama utakuwa nami hata kwa macho ....hakika ni kazi ya mikono yangu mwenyewe..naPENDA SANA KUCHANGANYA CHANGANYA UDOGO NA MIKONO YANGU....
ReplyDeleteDuh,....kweli nii uandilizi wa kisasa, maana ukiangalia picha pekeee kuacha hiyo ya miche,unaweza ukazania ni sehemu inaandaliwa kwa mashambulizi ya kivita.HONGERA MPENDWA
ReplyDeleteKazi nzuri sana Yasinta. Mie nasubiria maboga na mboga zingine na safari hii ntakuja tu kwako kuzifaidi na ugali. Jamani unga wa ugali uliotoka nao Tanzania nadhani utakuwa haujaisha. Haya na kuhusu bustani ya maua ni nzuri sana ila mie nna swali je hayo maua uliyapanda lini? Mana yanaonekana kuwa yana kamuda kidogo na wakati hali ya hewa ilikuwa sio nzuri na imekuwa safi wakati huu huu? Au huwa unasiri na maua kama ulivyofanya kwenye miche ya maboga na nyanya? Mkulima haswa wewe nadhani familia yako inafurahia kuwa na mama kama wewe. Siku njema Yasinta.
ReplyDeleteSafi sana, nitakuja kukutembelea wakati wa kuvuna hahaa.
ReplyDeletehaya dada mchicha vp?.natumai kutumiwa japo kafungu kamoja cha majani ya maboga hapa
ReplyDeleteHongera KADALA..Niliyotaka kuongea..Mwanakwetu...da'Edna na kaka wa mimi Isaakin..wameniwahi..Sasa sijui Ujanja kuwahi au Kupata?.
ReplyDelete@Ndugu WA mimi Eme wa 3 UMENIFANYA NIKAUKE KWA KICHEKO....hahahahhah
Usiye na! Kwanza ahsante. . Na halafu karibu saba unga bado upo wala usikonde ila pilipili mbuzi ndo naotesha sijui zirakuwa tayari? ...kuhusu maua ni kwamba yapo kama vitunguu baridi ikipungua yanachipua. ...itabidi niandike kiyu kuhusu hii siku moja. ..natumai umeelewa.ningejya jinalo ningekuwa na furaha kweli.
ReplyDeleteEdna! Itakuwa furaha isiyo maelezo kwa kweli. .karibu
sana ..hata ukija kabla mavuno itakuwa bombi.
Kaka isaack! Hej! .. usikonde mchicha nitapanda. Nitakutumia magungu kumi na ya mboga za maboga kumi nipe add....
Kachiki...duh umenikumbusha nilimsahau ndugu wangu....kufanya hivyo bustani kunazuia nyasi pis maumivu ya mgongo.
ReplyDeleteKachiki!... njoo nsaidie. ..na najua una mengi ya kusema!!
Vizuri, ila usipande zile mboga za CHAINIZI kwani zinauwa Mbegu za kiume kwa sis wanaume.
ReplyDeleteDuniani kila mtu na talanta yake!
ReplyDeleteUbunifu huu unatoka ndani, si wa kuigiza..
Swali, ulipofunika pana siri gani?
Duh! Usiye na jina sasa abalso najua wewe ni mwansume...sawa naheshimu ushauri wako sitapanda.
ReplyDeleteMija dada mkuu msaidizi wangu..hapa nolipofunika ni kuua nyasi. Yaani uliweka plastiki kqenye nyasi zinakufa natumai umenipata.
Hongera sana kwa kazi njema na Mungu akubariki sana!!
ReplyDeleteKaka RAy! Ahsante sana . Ubarikiwe nawe pia
ReplyDeleteMie nisiye na jina wa May 16, 2013 at 5:19 PM. Mie ni dada. Huyo mwingine aliyeandika kuhusu chinizi sio mimi. Haya Dada endeleza kilimo kwanza.
ReplyDeleteOh! kumbe wewe ni mdada...aise ningependa kweli kujua jinalo..Kilimo mtindo mmoja si unajua mtoto wa nyoka ni nyoka:-)
ReplyDeleteHaya dada wa mimi ninakuja kukusaidia na kujifunza zaidi...
ReplyDeleteKachiki raha jweli ngoja tutaimba na wimbo huu Chama chama chiwuyayi.×2 chiwuyayi ×2. Unaufahamu?
ReplyDeleteMie unanifahamu mbona sana tu! Ngoja ntakwambia nani mie kwenye simu. Mh nimekumbuka ile anwani yangu nimeipata ya kunitumia chakula ila sasa hakuna tena lasagne! Oh ntakutumia ili vikiiva unavyolima unitumie wakati najiandaa kuja kwako. Jioni njema.
ReplyDeleteHongera inaelekea haya ni matunda ya elimu ya Kujitegemea ya Enzi hizo katika shule za msingi.
ReplyDeleteWakati huo kulikuwa na bustani shuleni na kila mtu alikuwa na matuta yake ya kumwagilia na tulikuwa tunakwenda na vyambo vya kumwagiliaji maji pamoja na maji hata kama mvua imenyesha
Kila la kheri.
Mmmmmh..usiye na jina kweli nakufahamu kweli? hahaaaaa hiyo anwani inaonekana mpaka uitolee pesa...haya mie nasubiri:-)
ReplyDeleteKaka Salehe,umenikumbusha mbali nimecheka kweli kweli. Ahsante kwa kumbukumbu.
Kutunza Bustani Kwaweza Kukunufaisha
ReplyDeleteJE, WEWE hufurahia kutunza bustani? Huenda unanufaika hata zaidi kutokana na utendaji huo. Kulingana na gazeti moja la London (Independent), watafiti wamegundua kwamba “kutunza bustani hukusaidia kuwa na afya nzuri zaidi, hupunguza mifadhaiko, hushusha shinikizo la damu na hata kukusaidia kuishi kwa muda mrefu zaidi.”
Mhariri Gay Search anasema: “Baada ya siku yenye shughuli nyingi na mambo mengi yenye kufadhaisha, kurudi nyumbani na kutunza bustani yako huburudisha sana.” Mbali na kuwa jambo lenye kuthawabisha na kupendeza, kutunza bustani kunakuwezesha kupata mazoezi mazuri zaidi ya mwili kuliko kwenda katika chumba cha mazoezi. Jinsi gani? Kulingana na Search, “utendaji kama vile kulima na kukusanya majani ni mazoezi mazuri yanayotumia kalori nyingi zaidi kuliko kuendesha baiskeli.”
Kutunza bustani huwanufaisha hasa wazee. Kusubiri chipukizi au mche mpya uibuke huwasaidia kutazamia wakati ujao wakiwa na uhakika. Pia, “bustani hutuliza maumivu na mfadhaiko” unaosababishwa na uzee, asema Dakt. Brigid Boardman wa Royal Horticultural Society. Mara nyingi wazee huvunjika moyo kwa sababu ya kuwategemea sana wengine. Hata hivyo, kama Dakt. Boardman anavyosema, “ile hisia ya kutaka kujitegemea inatoshelezwa kwa kuamua kitakachopandwa, mahali kitakapopandwa, na jinsi ya kuitunza bustani. Na ule uhitaji wa kutunza unatoshelezwa pia.”
Wale walio na matatizo ya akili mara nyingi hutulia wanapofanya kazi katika mazingira mazuri, matulivu. Isitoshe, kupanda maua au chakula kwa ajili ya wengine kwaweza kuwasaidia watu hao wajiamini tena na kujiheshimu.
Hata hivyo, wanaofaidika na bustani hizo si wale wanaozitunza tu. Profesa Roger Ulrich wa Chuo Kikuu cha Texas alifanya majaribio kwa kutumia kikundi cha watu waliokuwa wametiwa chini ya mkazo. Aligundua kwamba wale waliopelekwa mahali penye miti na majani mengi walipata nafuu haraka—kulingana na mpigo wa moyo na shinikizo la damu—kuliko wale ambao hawakuwekwa katika mazingira hayo ya asili. Jaribio kama hilo lilionyesha kwamba wagonjwa wanaoendelea kupata nafuu katika hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji walinufaika kwa kukaa katika vyumba ambamo wangeweza kuona miti. Tofauti na wagonjwa wengine, “walipata nafuu haraka, wakarudi nyumbani mapema, hawakuhitaji dawa nyingi za kutuliza maumivu, na walikuwa na malalamiko machache zaidi.”_jw.org
Mimi nigardencolic yaani nimependa hayo maua mpendwa yanaitwaje?na yanachukua muda gani kuchanua maua,hongera sana
ReplyDelete