Hapa
Sweden leo ni siku ya akina mama duniani. Nasi leo tumeamua kumpongeza mama yetu
mpendwa ktk blog yake ni sisi Camilla na Erik. Tunampenda sana mama yetu hasa
akiwa na hasira, huwa tunapata kila kitu tutakachotaka/omba.( kwa niaba ya mama)
Ok, basi nami nimepata nafasi ya kusema machache ni kwamba. Najua sehemu
nyingine siku hii imeshapita ila hapa Sweden ni leo. nami napenda kuwapa pongezi
akina mama wote duniani bila kumsaau mama yangu. NAWAPENDA AKINA MAMA WOTE
DUNIANI.NA TUTAFIKA TU.
Hongera Dada Yasinta na wamama wote duniani! Tunasubiria leo mapishi kwa hamu utakayowapikia hapo nyumbani mana ni siku yako, au leo unapumzika baba na watoto ndio wapishi? Kama utapika madiko diko tuwekee hapa angalau tule kwa picha tu, mana nasikia njaa! Siku njema.
ReplyDeleteAhsante usiye na jina. Leo ni siku yangu hakuna kupika nitapikiwa...yaani raha kweli:-)
ReplyDeleteHongera kupikiwa nilidhania utaingia kupika. Tunashukuru kuona keki nzuri ya Dada Camilla. Na hongera kupata zawadi kem kem.
ReplyDeleteSiku moja kustarehe si mbaya...nilifurahia kila dakika...ndiyo keki ilikuwa tamu sana. Bahati mbaya ulishindwa kuja:-)
ReplyDeleteShukran na Hongera sana
ReplyDelete