Thursday, April 4, 2013

TUSISAHAU METHALI ZETU....!!!!!

1. Watu tunawadhania ni marafiki, mara nyingine ni maadui.. Mpelelezi si rafiki.
2. Mtu akitaka kupata cheo, awe na heshima kwa wakubwa.
3. Kama ukipata mali kwa kazi yako, weka akiba kwa siku za uzee.
4. Ufuate mashauri na maneno ya watu wenye akili.
5. Mtu ana maneno mazuri na matamu, lakini nia yake ni mbaya.
6. Ukiwa mgeni katika nchi, uelekee kadiri watu walivyo.
7. Wakiwa wakubwa wawili, watapata ugomvi, hawawezi kukaa pamoja.
8. Mtu akitangaza habari ya uongo, ni vigumu kusahihisha maneno yake.
9. mtu anaweza kukuchekelea kwa mdomo, lakini katika moyo ana mawazo mengine.
10. Ujitahidi mwenyewe na Mungu atakusaidia.
TUTAENDELEA KUKUMBUSHANA KILA WIKI ILI TUSISAHAU..NA KAMA KUNA MMOJA ANA NYINGINE ANAWEZA KUONGEZEE TU...SIKU NJEMA SANA PANAPO MAJALIWA TUTAONANA TENA...KAPULYA

8 comments:

  1. Hizi methali zimebeba ujumbe wenye hekima na busara ndani yake, wazee wetu walisema hayo maneno wakijua ukweli halisi wa mambo hayo katika jamii yetu. Ahsante dada Yasinta kwa kutunoa kimaarifa.

    ReplyDelete
  2. Kaka said! Ahsante sana...tupo pamoja ndugu yangu.

    ReplyDelete
  3. Karibu Kachiki. ..wote tuna nia moja.

    ReplyDelete
  4. 1.Mpanda mti atashuka, hawezi kukaa huko milele.
    2. Ukipendacho wewe, sio lazima kila mtu akipende.
    3.Usimcheke mzee, kwani ipo siku na wewe utaufikia, kama ikibahatika.

    Nimekokotoa hizi, kwani nimeona hizo za kwako zipo katika mfumo huo. Tupo pamoja ndugu wangu

    ReplyDelete
  5. imetulia sana
    www.supermzigo.blogspot.com

    ReplyDelete
  6. Matumizi ya metahali na nahau ni uthibitisho wa uwezo wa wadau katika kulinda na kuhifadhi hazina ya lugha ikiwa sehemu muhimu sana katika utamaduni wa jamii husika.

    ReplyDelete
  7. vimax thanks gan infonya vimax asli di tunggu info selanjutnya gan obat klg

    ReplyDelete