Wednesday, April 10, 2013

PICHA YA WIKI:- WANAWAKE WANAWEZA HATA KABLA HAWAJAWEZESHWA.....

Hapa nimejiuliza mara kumi kumi hivi anawezaje  huyu mama....maana kuendesha baiskeli unahitaji balansi na kuubeba huyo mzigo pia halafu mtoto mgongoni na mtoto nyuma ya baiskeli naye kabeba mtoto ...mmmmhhh hapa kazi  kwelikweli....Lakini kweli hii ni haki kweli/Uungwana kweli??? KILA LA KHERI !!!

10 comments:

  1. Huyo bi mkubwa anaonekana kuwa sugu na fundi kweli kweli. Hata hivyo tusimshangae. Mara nyingi mazingira humfinyanga binadamu akaenda nayo sambamba. Huenda hata da Yacinta ungekuwa kwenye viatu vyake saa nyingine ungekanyaga pedal kwa ufundi zaidi yake.

    ReplyDelete
  2. Shida zinafundisha mengi Yasinta hasa yasiyowezekana kwenye shida huwezekana! Je dada yetu hujawahi kupata shida kubwa hapa duniani ambayo imekufanya ukafanya vitu ambavyo ni vgumu kuamini? Au uko kwenye mafanikio tu na shida umezisahau? Mie sishangai kabisa Mungu atusaidie kina mama.

    ReplyDelete
  3. Nikirejea swali lako Yasinta la Je ni haki kweli kwa mwanamke huyu kuwa katika hali hii...

    Yasinta duniani kuna watu wa aina tofauti tofauti mimi nimeshakutana nao. Utamkuta mtu yuko katika hali ngumu ya kuhitaji msaada lakini ukithubutu tu kutaka kumsaidia utashangaa atakavyokukwepa...Attention seekers!!
    Hawa hutafuta kuhurumiwa na jamii au kupewa sifa kwamba wanaweza kila kitu.

    Kwa hiyo hata huyu mama huwezi kujua nini kimesababisha kubeba vyote hivi kwa mara moja, labda ni mmoja wa wapenda sifa au wanaopenda kusikia maneno ya huruma na faraja au labda ni kweli hali yake ya maisha ni ngumu.

    Lakini All in all huyu mwanamke anatufundisha kuwa binadamu tuna uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo zaidi ya ambavyo tunadhani.

    Ni hayo tu kwa sasa..

    ReplyDelete
  4. Ni kweli inabidi iwe hivyo,maana uchungu wa mwana aujuaye ni mzazi

    ReplyDelete
  5. Dada Shikamooo

    Nimerudi mwanampotevu

    naahidi sitapotea tena

    ReplyDelete
  6. Ndomaana ,nakataa kuamini kuwa wana wake hampendani.Angalia mlivyo muonea huruma mwanamke mwenzenu kutokana na muonekano wake katika picha hii. mimi kwa ufahamu wagu nina amimini huyu mama/mwanamke anaonekana hivyo kutokana na mazingira yalivyo au yaliyo mzunguka.na wala sidhani kama anadhiki,au shida kimaisha. angaloa jinsi alivyo vaa.msisahau mifumo wanayo kulia baadhi ya wanawake ndiyo inayo sababisha kufikiria hivyo mnavyo fikiria ,kwamba yawezekana anateseka, kumbe waweza kuta, kwake nikitu cha kawaida,hivyo kuanza kutafuta namna ya kumsaidia mkidhani ndo kumkombowa ,bila kujuwa chanzo .hebu kila mtu ajikumbushe kwa wale tuliozaliwa vijijini kabla ya kuja mjini ,hali ilikuwaje mama zetu kwa wale ambao walikuwa ni wamama wanyumbani masaa yote na siya waajiliwa ilikuwaje maisha hapo nyumbani.mimi mama yangu alikuwa si mfanyakazi,nikikumbuka sasa, naonakabisa alivyo kuwa akijituma katika kilimo pamoja na mzee/baba yangu kuwa na kazi nzuri naya maana wakati huo kama mwalim mkuu washule ,alifanya shughuli nyingi sana mama yangu ambazo kama nilivyo sema ukizifikiria kwa sasa waweza sema labda baba hakumsaidia kupunguza mizigo hiyo/shughuli hizo.kaka s

    ReplyDelete
  7. Duhhh hapa nimejifunza mengi..asante da'KADALA kwa hili....

    lakini dadake....teh teh tehhh[kujinyanyasa au..]

    ReplyDelete
  8. Uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!
    Ni nani kama mama?
    Hakika kila mtu anastahili kulia mama yangu au....................!!
    Hakika mama ni nguzo ya dhahabu isiyoisha thamani.
    Pongezi kwa matiti tuliyonyonya na mikono salama iliyotulea.
    Salamu kwako Yasii na wadau wote wa kibaraza chako chema sana.Chema chajiuza kibaya..........................!!

    ReplyDelete
  9. Nachukua nafasi hii kwa kuwashukuruni wote kwa mchango wengu kwa wanamke...Na paia nachukua nafasi hii kumkaribisha mwanampotevu mdago wangu wa Hiari Koero ambaye alikuwa amepotea kwa zaidi ya mwaka sasa. KARIBU SANA :-)

    ReplyDelete
  10. Hongera sana mwanamke..........tena yupo ngangali kweli kweli lengo afike/awafikishe aendako salama na mizigo yake yote

    ReplyDelete