Leo nimeulizwa swali hili ..ilianza hivi:- Kuna swali linanisumbua katika kichwa changu ngoja niulize ili tusaidiane...haha hivyo nikashindwa lakini nikakukumba kwenye wengi hakiharibiki kitu. Na swali lenyewe likawa kama ifuatavyo:- Laiti jana ingekuwa kesho, leo ingekuwa Ijumaa. Je? mwalimu aliyasema haya siku gani?
Pole sana... hili swali ukilijadili sana kichwani mwako utaumia. Jibu ni Alhamis
ReplyDeleteAlhamisi
ReplyDeleteInasikika kama Alhamisi?Wadau wengine sijui naona tupo pamoja au wana jipya?Acha tuone!!
ReplyDeleteCathbert, Amina na Ray ...asanteni sana kwa kupita hapa na kuacha yenu yaliyo moyoni...pamoja daina....
ReplyDeleteNi siku yoyote, kwani hata hilo dokezo la siku ya Ijumaa limekaa kidhahania ...inge ... lakini siyo lazima iwe Ijumaa. Kwa hiyo. Unaweza kutumia swali hili kuhusu siku yoyote katika juma. Alhamisi ni moja wapo. Maana kinachotafutwa hapo ni siku aliyosema mwalimu.
ReplyDeleteSikh ya jumaili
ReplyDelete