Wednesday, March 20, 2013

MSIBA..DADA MARIANA HATUNAYA TENA...

 
 
 

 
Kama mnawakumbuka picha hii na tukio lake basi ni kwamba Dada mkubwa Mariana Kutoka nchini Angalo katika picha kushoto mwenye miwani katuacha ghafla leo . Ni masikitiko makubwa sana kwa familia yake marafiki na jamaa. Da Mariana alikuwa mtu mmoja ambaye ni mcheshi, makarimu na mwenye kupenda sana watu. Kwangu ni pigo kubwa sana, kwani yeye alikuwa mtu muhimu sana kwangu, zaidi ya rafiki...alikuwa hakosi kunifariji pale nilipokuwa na matatizo.. nimepatwa na mshtuko wa ajabu kwa kweli...hebu soma hapa. MWENYEZI MUNGU NA AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI...AMINA

14 comments:

  1. Pole kwa kufiwa na dada Mariana - MWENYEZI MUNGU NA AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI...AMINA
    By Salumu.

    ReplyDelete
  2. Pole sana dada kwa kufiwa na ndugu yako wa karibu najua inauma sana lkn yatupasa sote kumuombea mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.

    ReplyDelete
  3. Pole sana Yasinta, Mungu azidi kukufariji.

    ReplyDelete
  4. Ghafla kivipi Yasinta, aliumwa ghafla au?...aisee nami ni mmoja wa walioshtuka..

    Poleni sana Mungu awatie nguvu.

    Amen.

    ReplyDelete
  5. Poleni sana kwa msiba Da Kapulya. Mwenyezi Mungu awatie nguvu na kuwaimarisha katika kipindi hiki. Apumzike kwa amani, Mariana.

    ReplyDelete
  6. Pole kwa dada Yasinta na kwa ndugu jamaa na marafiki.Daima urafiki unashinda undugu.

    ReplyDelete
  7. Pole! dada Yasinta kwa kuondokewa na mtu muhimu sana kwako. Mwenyezi Mungu akupe nguvu na moyo wa amani.

    ReplyDelete
  8. Nachukua nafasi hii kwa kupenda kuwashukuru wote mliokuwa nasi katika kipindi hiki cha majonzi. Mmetupa nguvu za aina yake ..Ahsanteni sana nitawajuza lina mazishi yatafanyika.Mungu awabariki na ampokee Mariana na kuiweka roho yake mahali pema peponi. Amina.

    ReplyDelete
  9. Pole sana rafiki yangu, Mungu akutie nguvu kipindi hiki upate kumuombea dada Mariana roho yake ipumzike kwa amani, na pia uweze kuwafariji watoto wake, maana watakua wanakuangalia wewe, sasa wewe ukiwa mmnyonge ni nani atawatia moyo?

    ReplyDelete
  10. Rafiki! ahsante kwa pole na pia kwa maombi yako. Na hasa kwa ushauri ni kweli inabidi nijikaze kwelikweli..hata kama si rahisi.

    ReplyDelete
  11. Poleni sana..MUNGU awatie nguvu katika wakati huu mgumu kwenu.

    ReplyDelete
  12. Pole sana kwa kuondokewa na rafiki mpendwa.

    ReplyDelete
  13. Kachiki hakika nahitaji sana sala hizo Ahsante ndugu wangu.

    Edna, Ahsante sana..

    ReplyDelete
  14. pole sana my dada ulikuwa unatia huruma sana ila yote ni ya MUNGU

    ReplyDelete